Home Audio Wasanii waaswa kuendeleza ushirikiano baina yao na Serikali

Wasanii waaswa kuendeleza ushirikiano baina yao na Serikali

SHARE
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mashirikisho ya wasanii Tanzania, Basata, Haak Neel Production, Bodi ya Filamu na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa hafla kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii wikiendi hii jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifamba mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akihutubia mbele ya wadau wa sanaa (hawapo pichani)wakati wa hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Haak Neel Production waendeshaji wa maonyesho hayo Bw. Namala (katikati) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel mara baada ya kumaliza hotuba yake katika hafkla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi.

Wasanii wa kikundi cha Dar Creative wakionyesha moja ya kazi zao wakati wa hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii wikiendi hii jijini Dar es Salaaam.


Wasanii wa kikundi cha T-Afrika wakionyesha moja ya kazi zao wakati wa hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii wikiendi hii jijini Dar es Salaaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkabidhi tuzo ya heshima ya sanaa za maonyesho Bw. Bakar Mpelembe (Mzee Jangala) wakati wa hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

: Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkabidhi tuzo ya heshima ya sanaa ya Muziki Bi Shakira wakati wa hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii waliopewa tuzo za heshima kutokanma na mchango wao katika fani zao. Kutoka kushoto ni Jacob Steven (JB) ambaye amemuwakilisha mshindi wa tuzo ya heshima katika sanaa ya Filamu Bibi. Tecla Mjata, Bakar Mpelembe (Mzee Jangala) aliyepewa tuzo ya heshima ya sanaa za maonyesho, Bi. Shakira ambaye amepewa tuzo ya heshima ya sanaa ya Muziki na Bw. Robert Jacob aliyepewa tuzo ya heshima katika sana za ufundi.Tuzo hizo zimetolewa na wakati wa hafla ya kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

Wasanii wa kikundi cha Dar Creative wakiwa katika zulia jekundu maalum kwa ajili ya watu mashuhuri kupiga picha wakati wa hafla kufunga maonyesho ya Siku ya Msanii wikiendi hii jijini Dar es Salaam.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

SHARE