Home Audio
SHARE

NI
SOO! Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Moshi Katemi maarufu kama Mo
Music, ametiwa mbaroni mjini Dodoma kwa madai ya utapeli wa mamilioni ya
shilingi ya kigogo anayetajwa kwa jina moja la Barthazar, ambaye ni
mhadhiri wa Chuo cha Mipango cha mjini humo.

Kwa mujibu wa chanzo
cha kuaminika, ishu hiyo ilitokea wiki iliyopita baada ya kuhusishwa na
msichana aitwaye Joyce Ngerangera ambaye awali alikuwa ni mpenzi wa
mhadhiri huyo.

Inadaiwa kuwa Mo Music alikamatwa wakati akitoka
nje ya Studio ya Radio Free Africa jijini Dar es Salaam kwenye
mahojiano, ambapo makachero waliotumwa kutoka Dodoma, walimtaka aende
Kituo cha Polisi Oysterbay.

“Walikwenda naye kituoni na baadaye
akasafirishwa kwenda Dodoma ambako alitoka kwa dhamana, kesi yake
ilihusiana na kupewa pesa na Joyce ambaye alikuwa akizichuma kwa
Barthazar, jamaa alichukia baada ya kubaini kuwa licha ya kuchukuliwa
fedha zake, pia Mo alikuwa akitembea na demu huyo,” kilisema chanzo
hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Mo Music ambaye alifunguka kuwa ni
kweli alikamatwa kwa ishu hiyo, lakini akasema haelewi lolote zaidi ya
ukweli kuwa kwa kipindi kifupi, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
Joyce.

“Huyo demu nilishaachana naye kitambo tu, sasa kilichopo
ni kwamba huyu mwanamke alimchezea mchezo jamaa, siku moja wakati
wakifanya yao kwenye gari, demu aliwaita watu wakajifanya polisi,
wakawapiga picha na kumwambia huyo mwanaume awape pesa la sivyo
watamchafua, ikabidi awape milioni mbili.

“Sasa kila baada ya
muda alikuwa akichukua simu ya mtu yeyote na kujifanya ndo wale maaskari
awape pesa, naye anatuma, siku moja alichukua simu yangu akasema kuna
mtu atamtumia pesa maana simu yake imezima chaji, ikatumwa laki na nusu,
mimi sijui kama ni dili anacheza, cha ajabu baada ya kushtukia hiyo
ishu, jamaa anadai mimi ndiyo nahusika na mchezo mzima hivyo ananidai
milioni thelathini na nne alizotapeliwa wakati sihusiki kabisa,”
aliongeza Mo Music.

Kwa upande wake Joyce alikiri kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na Barthazar uliodumu kwa mwaka mmoja kabla ya
kushindwana na yeye kuanza na Mo Music.

“Kinachomsumbua ni wivu
kisa nimeachana naye, kama ni kesi angetakiwa adili na mimi, siyo Mo
Music, anamuonea tu, hahusiki hata kidogo kwenye hiyo ishu,” alisema.
Barthazar
alipotafutwa, alisema hawezi kuiongelea kesi hiyo iliyofunguliwa jalada
namba DOM/IR/6365/2015 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, kwa kile
alichosema kuwa kesi hiyo imefunguliwa na Jamhuri hivyo hawezi
kuiongelea, labda kama ataulizwa msanii huyo.

CREDIT: RISASI JUMATANO

SHARE