Home Audio Video: Afya ya Mugabe yazidi kuwa utata baada ya kutaka kuanguka hadharani...

Video: Afya ya Mugabe yazidi kuwa utata baada ya kutaka kuanguka hadharani India

SHARE
http://www.timeslive.co.za/incoming/2015/11/01/mugabe.jpg/ALTERNATES/crop_630x400/Mugabe.JPG
Maafisa wa nchini Zimbabwe wamekanusha tetesi za kuwa afya ya Rais
Robert Mugabe imezidi kuwa mgogoro baada ya Jumamosi kukaribia kuanguka
hadharani.Mugabe alionekana akipepesuka wakati alipokuwa akipanda jukwaani katika mkutano wa India na Afrika wiki hii.


Video zilizosambaa mtandaoni zinamuonesha waziri mkuu wa India Narendra Modi akimsaidia kumshika mkono Mugabe mwenye miaka 91.
Msemaji wa rais, George Charamba alisema kuwa hilo ni tukio dogo tu.
“Rais hajambo na amekamilisha azma yake,” alisema.
Mapema mwaka huu, Rais Mugabe aliteleza na kuanguka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa nchini Zimbabwe.

CHANZO:bongo5.com

LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

SHARE