Home Audio KAMATI KUU YA CCM YAPITISHA MAJINA MATATU YA WAGOMBEA USPIKA,SITTA NCHIMBI CHALI

KAMATI KUU YA CCM YAPITISHA MAJINA MATATU YA WAGOMBEA USPIKA,SITTA NCHIMBI CHALI

SHARE
post-feature-image

Majina hayo yamepenya kutoka katika orodha ya majina 21, miongoni mwao
akiwemo Spika wa Bunge la 9, Samuel Sitta, Dkt. Didas Masaburi ambaye
alitangaza kujitoa katika dakika za mwisho, Dkt Kalokola na wengineo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni ya leo baada ya kikao cha Kamati
Kuu kilichoongozwa na mwenyekiti wake Dkt Jakaya Kikwete mjini Dodoma,
jina moja kati ya hayo matatu litatangazwa kesho Jumatatu ikiwa ni
pamoja na jina la mgombea wa nafasi ya Naibu Spika.
Katika waliopitishwa:
Job Ndugai ni mbunge mteule jimbo la Kongwa Dodoma na pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge lililopita.
Dkt Tulia Ackson ni Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali, pia alikuwa ni
mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akitokea taasisi za elimu ya juu.
Amekuwa mhadhiri wa sheria katika kitivo (sasa shule) cha sheria chuo
kikuu cha Dar es salaam.
Abdullah Mwinyi ni mtoto wa Rais mstaafu Al Hajj Aly Hassan Mwinyi na ni mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.


Wana-CCM
hao watatu watapigiwa kura na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM
kitakachofanyika kesho Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za
Makao Makuu ya CCM Dodoma ilikuchagua jina moja kugombea nafasi hiyo
katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kuhusu nafasi ya Naibu
Spika, alisema kulikuwa na kasoro za kutofuata kanuni za chama ambapo
hadi jana ni mwanachama mmoja tu ndiye aliyekuwa amechukua fomu ya
kugombea ambaye ni Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu,’ lakini
atatakiwa kuchukua fomu upya.

“Ibara ya 57, Kanuni za kamati ya
wabunge wote wa CCM toleo la 2010 toleo la nne 2011, mbunge yeyote
anayetaka kugombea nafasi ya Naibu Spika atatakiwa kuchukua fomu kupitia
kamati hiyo na atairudisha kisha kamati itakaa kupata jina moja,”
alisema Nape.

Kwa mujibu wa maelezo hayo mbunge wa chama hicho
anayetaka kugombea Unaibu Spika, atatakiwa kuchukua fomu leo Novemba 16,
kwa ada ya Sh 100,000 kisha atairudisha kesho Novemba 17, ndipo kamati
itakaa kuchambua na kupitisha jina moja.

Je, Nani kati ya hawa watatu apewe nafasi na CCM?

        

USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

SHARE