Home Audio TUME YA UCHAGUZI YAFUNGUKA KUHUSU WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU...

TUME YA UCHAGUZI YAFUNGUKA KUHUSU WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU UJAO

SHARE
http://2.bp.blogspot.com/-3_xQY2KDAvw/VKZx0zfQS7I/AAAAAAAAGtQ/jSG1nDjvbp0/s1600/hjuma.JPG
Tukiwa bado tupo kwenye headlines za Uchaguzi 2015 leo Octoba 7, 2015
Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva ametolea majibu
kuhusu Wanafunzi kushiriki Uchaguzi mkuu.
‘Suala la Wanafunzi mara kwa mara limekuwa likiletwa na sisi kwenye tume
tumesema kwamba linafanywa kama la kisiasa kwa maana kwamba mara kadhaa
wanafunzi walipokuja pale ofisi za tume kile kikundi chao wakatuambia
kwamba kipindi hiki watakuwa likizo‘ Lubuva

‘Tukawapa ushauri na tukazungumza nao nimeenda mpaka chuo cha Dodoma
tukazungumza nao na tukawapa utaratibu mpaka tukaunda kamati ikaongozwa
na Jaji Mkwawa wasikilizwe wakaelezwa na baadae wakaandikiwa barua kwa
hiyo hili suala ni suala la kisiasa na tumeshughulika nalo mwisho
tukawaambia kwamba wamejinyima wenyewe hii nafasi’- Lubuva

‘Kwa hiyo suala la wanafunzi ninasema kwa niaba ya wenzangu kwamba
kwenye tume tumefunga mlango na upande wa kuboresha daftari umepita ni
wao wenyewe wamejinyima na kuhusu kwamba vyuo vifungwe kwasababu ya
Uchaguzi Mkuu ni suala la Wizara ya Elimu sio la tume ya Uchaguzi –
Lubuva

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Jaji Damian Lubuva

SHARE