Home Audio TAZAMA VIDEO RAIS KIKWETE AKIWA MKUU WA MAJESHI DAVIS MWAMUNYANGE KATIKA...

TAZAMA VIDEO RAIS KIKWETE AKIWA MKUU WA MAJESHI DAVIS MWAMUNYANGE KATIKA UZINDUZI WA UWANJA WA NDEGE ZA VITA MOROGORO

SHARE

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais JAKAYA KIKWETE amezindua awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege za vita uliopo katika kamandi ya jeshi la anga iliyopo NGERENGERE mkoani MOROGORO.

Akizindua ujenzi huo,Rais KIKWETE amesema mazingira bora ya uwanja huo pamoja na kutumika kwa shughuli za kijeshi, yatawawezesha watu kufanya kazi kwa bidii na kuchochea uboreshwaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. HUSSEIN MWINYI amesema kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni hazina kwa jeshi la wananchi na taifa zima huku akisisitiza suala la matumizi ya uwanja huo kuboreshwa.
Naye Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali DAVIS MWAMUNYANGE ameeleza mikakati iliyopo ya kuboresha jeshi hilo, huku mkuu wa jeshi la anga Meja Jenerali JOSEPH KAPWANI akisema uwanja huo utakuwa bora katika nchi za Kusini mwa AFRIKA.

Mradi huo utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milion 68 hadi utakapokamilika na unafadhiliwa na serikali ya CHINA ambapo katika awamu ya pili mita 600 zitaongezwa na hivyo kufanya uwanja huo kuwa na mita 3000 mara utakapokamilika.
Link hiyo hapo chini ukitaka kumuangalia. 

Chanzo: TBC1
SHARE