Home Audio TANZIA: Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini Afariki Dunia

TANZIA: Mgombea Ubunge wa Arusha Mjini Afariki Dunia

SHARE

Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo  Ndugu
Estomih Malla amefariki dunia usiku wa leo saa saba katika hospitali ya
KCMC Moshi.

Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas
iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya
kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.

Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika
mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika
kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo
madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo
anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.

Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha
kutokea kwa kifo hicho. Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya
uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani
Arusha.
Chanzo:Times Fm

SHARE