Home Audio Siku Nane zatolewa kuhakiki taarifa kituo cha kupigia kura

Siku Nane zatolewa kuhakiki taarifa kituo cha kupigia kura

SHARE

Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva,
akizungumza na wahariri vyombo vya habari Dar es Salaam. Kulia ni
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Julius Mallaba. 
Na Anitha Jonas-Maelezo
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi  yawaasa  wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa
zao katika vituo vya vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi.

Hayo
yamesema jana  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian
Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya
siasa uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,
Jaji
Lubuva amesema kuwa lengo la mkutano huo ni  kushauriana na vyama vya
siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25
mw`aka huu.
“Tume
imepanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura 
anapata haki ya kupiga  kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi
za upendeleo kwa watu wenye ulemavu  wa aina mbalimbalina na imeandaa
karatasi maalum za kupigia kura kwa watu wenye walemavu wa
kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha
Jaji Lubuva aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala
ya kuilalamikia Tume katika majukwaa  wakati wa kampeni  pia amewasaa
wanasiasa hao  kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha
kukimbilia waandishi wa habari.
Mbali
na hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi
wa vyama vya siasa wanao walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo
vya kupigia kura kuacha kauli hizo kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba
wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani kuwa jumla ya watu 3,870
walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao
vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la
kudumu la kupiga kura.
“Katika
kuelekea uchaguzi  Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105 ambapo
Tanzania Bara ni vituo 63,525 na Zanzibar  ni vituo 1,580 kila kituo
kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wapiga kura 450 na kituo kitakacho kuwa
na wapiga kura zaidi ya 500 kitagawanywa katika vituo viwili,”alisema
Bw.Ramadhan.
Mpaka
sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa
ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu,
karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila
vinatarajiwa kuisambazwa hivi karibuni.
SHARE