Home Audio
SHARE
SERIKALI
imejipanga kumaliza madeni inayodaiwa na walimu kwa awamu, ambapo zaidi
ya Sh bilioni 1.7 zitaanza kulipwa kuanzia wiki ijayo na kutekeleza
muundo mpya wa utumishi, ambao ni pamoja na kupandisha vyeo. 
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Utumishi, Hab Mkwizu
alisema madeni ya mishahara ya kuanzia Desemba 2013 hadi Agosti mwaka
huu, yanahusu walimu 60,322 sawa na madai ya Sh bilioni 29.8
yaliyowasilishwa kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kwa ajili ya
uhakiki na tayari halmashauri 103 zimeshahakikiwa. 
Alisema
uhakiki wa halmashauri zilizobaki unatarajiwa kukanilika Oktoba 11
mwaka huu na fedha zote zitatumwa kwa halmashauri husika mara baada ya
uhakiki kukamilika. 
Kati
ya kiasi hicho cha fedha wanazodai walimu, Sh bilioni 21 ni za waalimu
shule za msingi ambao ni 44, 715 na Sh bilioni 8.6 wa shule za sekondari
ambao ni 15,607. 
“Walimu
45,453 wanadai malimbikizo ya mishahara Sh bilioni 32 hadi kufikia
Septemba mwaka huu. Serikali ilikuwa imewalipa walimu 3,979 Sh bilioni
2.3 na wengine ambao bado wanadai watalipwa mwezi huu,” alisema Mkwizu. 
Alisema
madeni ya Sh bilioni 1.73 ya walimu 1,667 ndio yatalipwa mwezi huu huku
wengine wakiendelea kulipwa kila mwezi kadiri ya uhakiki unavyokamilika
na kwamba madeni yasiyohusu mishahara yamekuwa yakilipwa kupitia fungu
la matumizi mengineyo. 
Mkwizu
akifafanua madeni ya waalimu, alisema Serikali imeagiza pia kila
halmashauri kufanya vikao vya kuwapandisha madaraja walimu mapema
iwezekanavyo kabla ya Novemba mwaka huu. 
“Walimu
waliokaa kwenye cheo kimoja kwa muda mrefu na wale wanaokaribia
kustaafu watapewa kipaumbele katika upandishaji vyeo,” alisema Mkwizu.
SHARE