Home Audio MWALIMU MKUU ANASWA LIVE OFISINI NA MZAZI WAKITAKA KUVUNJA AMRI YA SITA...

MWALIMU MKUU ANASWA LIVE OFISINI NA MZAZI WAKITAKA KUVUNJA AMRI YA SITA YA MUNGU

SHARE
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar na mwanamke huyo.
DUNIANI kuna mambo! Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa iliyopo Upanga jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita alinaswa live ofisini kwake akiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mzazi wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, kisa kikitajwa ni maandalizi ya kuivunja amri ya
sita ya Mungu, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Tukio hilo la kufedhehesha, lilishuhudiwa na makamanda wa Global Publishers Kitengo Maalum cha Operasheni Fichua Maovu (OFM) ambapo pia watu wengine kadhaa walijionea kioja hicho cha mwaka.
HIVI NDIVYO ILIVYOANZA
Awali, Kamanda wa OFM akiwa kazini, alipokea simu kutoka kwa mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, akimfahamisha juu ya hali isiyo ya kawaida kwenye ofisi za mwalimu huyo zilizopo ndani ya geti la shule, kwani aliwaona askari polisi wakihaha kama wanaotaka kuzuia uhalifu.
“Jamani OFM, njooni hapa Shule ya Msingi Umoja wa Mataifa. Kama kuna ishu, naona askari wapo na pia ndani kwa mwalimu mkuu kama kuna ishu. Sijui ni nini!” kilisema chanzo hicho. Mara moja, kamanda huyo alifanya mawasiliano na wenzake waliokuwa ‘fildi’ na kuwafahamisha kuhusu ishu hiyo. Wakitumia pikipiki zao ‘zinazopaa’, makamanda hao walifika eneo la tukio dakika chache baadaye na kukuta mambo ndiyo kwanza yanaanza.

ENEO LA TUKIO
OFM walijitambulisha kwa askari waliokuwa eneo hilo na kuomba kwanza kupata picha kadhaa za kumbukumbu kabla ya maelezo, ndipo ndani ofisini, walimuona mwalimu huyo akiwa na taharuki huku akionekana kurekebisha vizuri suruali yake. Mbele yake alikuwepo mwanamke aliyejiziba uso kwa kutumia kiganja cha mkono mmoja.
SIKILIZA UTETEZI
Alipotakiwa kutoa maelezo ya kitu kilichokuwa kinaendelea ndani ya ofisi yake, mwalimu huyo alisema mwanamke aliye mbele yake alikuwa akitaka kumbaka, kwani aliingia ofisini humo na kuanza kujichekeshachekesha hovyo.
“Mkamateni mzazi huyo, anataka kunibaka. Kaja hapa, akaanza kujisemeshasemesha na kunifungua suruali yangu. Wakati namshangaa ndiyo nyinyi mnaingia,” alisema mkuu huyo huku akiichukua simu yake na kuonekana kama anayefuta kitu.
MWALIMU AWAKALISHA CHINI OFM, ASKARI
Hata hivyo, muda mchache baadaye, mwalimu huyo aliwaomba askari na makamanda wa OFM kukaa chini na kuyamaliza mambo hayo ili yasifike mbali.
“Jamani nyinyi ni wanaume wenzangu, mimi naomba tukae chini tuyamalize haya mambo hapahapa.”
OFM na askari hao walikataa mazungumzo hayo kwa vile kitendo cha mzazi huyo kukutwa ofisini muda huo ni chenye maswali mengi huku majibu yakiwa kiduchu.
MZAZI WA MWANAFUNZI ANENA
Akizungumza eneo la tukio, mzazi huyo (jina kibindoni), alisema kwamba alikuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa mwalimu huyo, akimtaka kimapenzi, jambo ambalo mara zote alikuwa akilikataa.“Huwa ananitaka, amekuwa akisema eti nikimfanikishia suala lake atahakikisha mwanangu anasoma vizuri. Sasa mimi hadi nimechoka. Wakati mwingine nilimdanganya nimesafiri. Siku moja nilifika hapa almanusura afanikishe kama siyo mlango wa ofisi kugongwa.”
USHUHUDA MZITO
Mwanamke huyo alisema siku hiyo alifika ofisini hapo baada ya kumuita, akimweleza kuwa alihitaji kuzungumza naye juu ya maendeleo ya mtoto wake. Hapo alipinga madai ya mwalimu huyo kuwa, alitaka kumbaka.
“Aaa! Kwa hili hawezi kukataa. Hata tukienda kwenye kampuni ya simu ninayotumia, tukaomba watutolee karatasi za kumbukumbu za nyuma (printout) simu ambazo tulikuwa tunapigiana utaona kwamba, alikuwa na mawasiliano na mimi ya muda mrefu sana. Kwa hilo asikatae, mimi sikutaka kumbaka ila yeye ndiyo alilazimisha penzi hapa ofisini.”
Wakati mwanamke huyo akitoa ushuhuda huo, mwalimu huyo alikuwa akisikiliza kwa umakini huku akiendelea kusisitiza utetezi wake.
MWALIMU APIGWA PINGU, OFM YAONDOKA
Baada ya hapo, OFM iliondoka ofisini hapo wakati mwalimu huyo akipigwa pingu. Na kwa mujibu wa askari, walikuwa wakienda kwenye kituo cha polisi kilicho karibu na eneo la tukio.

SHARE