Home Audio Mkapa Asema Mtu Anayehama Chama ni Msaliti na Hafai kuwa Kiongozi

Mkapa Asema Mtu Anayehama Chama ni Msaliti na Hafai kuwa Kiongozi

SHARE

RAIS
mstaafu Benjamin Mkapa amewaasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kuacha kambi ambazo ziliweza kusababisha majimbo mawili kuchukuliwa na
Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Lindi katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Rais
Mkapa aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa
chama hicho katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye
viwanja vya shule ya msingi ya Mpilipili mjini Lindi.
Alisema “acheni
tabia hiyo kwani mchakato wa kumpata mgombea inakuwa na utaratibu wake
na inapotekelezwa anapatikana mmoja ili apeperushe bendera ya chama”.
Mkapa
alisema wale wote ambao walishiriki kwenye kura za maoni za kumtafuta
mgombea ubunge, wanatakiwa kuwa wamoja wakishirikiana na yule
aliyeteuliwa kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa mwaka huu.
Alisema
kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu tabia hiyo iachwe mara moja ili
ushindi uwe wa CCM. Alisema mgombea anaposhindwa kwenye michakato hiyo
ndiyo anasema mfumo mbaya wakati wote yeye alikuwapo mwanzo mpaka
mwisho, akishashindwa anaamua kulalamika na kuhama chama.

Alimtaja mtu wa aina hiyo kuwa ni msaliti wa chama na hafai kuwa kiongozi.
 
Kiongozi
huyo mstaafu alisema mawaziri watatu waliokaa zaidi ya miaka 15 kwenye
serikali ya CCM kuanzia uwaziri hadi uwaziri mkuu na kuondoka wakidai
serikali hiyo haifai, wao ndio hawafai kuongoza nchi

SHARE