Home Audio
SHARE

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Mh. Jerry Silaa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Moshi Bar jimbo la Ukonga jijini Der es salaam wakati akiwaomba wananchi kumpigia kura za ndiyo ili awe rais na kuwatumikia watanzania.
Dk John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano huo amewaambia wananchi wa jimbo la Ukonga kuwa serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu Flying Over Tazara jijini Dar es salaam zenye thamani ya shilingi Bilioni 100 ili kupungunza foleni katika barabara za jijini Dar es salaam.
Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam ambapo wajenzi wa mradi huo ni kampuni kampuni ya Mitsui Costruction Ltd ya Japan na fedha zaidi ya shilingi bilioni 90 zimetolewa na Shirika la Maendeleo la Japan JAICA huku serikali ikichangia shilingi bilioni 8 za kitanzania ili kukamilisha mradi huo ambao utajengwa kwa miezi 35 mpaka kukamilika.(PICHA NA JOHN BUKUKU-UKONGA- DAR ES SALAAM)

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi Madiwani wa jimbo la Ukonga katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Moshi Bar jijini Dar es salaam.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Mh. Jerry Silaa wakipunga mikono na wananchi kwa pamoja.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik katikati Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam Simba Gadafi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida wakicheza nyimbo za hamasa katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika Viwanja vya Moshi Bar Ukonga leo.


Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wabunge wa jimbo la Dar es salaam viti maalum na mgombea ubunge jimbo la Ukonga Mh Jerry Silaa.

Mh. Diwani viti maalum jimbo la Ukonga Mama Tike Kitundu wa kwamza kushoto pamoja na madiwani wenzake wakanadiwa katika mkutano huo.

Umati mkubwa wa wananchi wa Ukonga na vitongoji vyake ukiwa katika mkutano huo.


Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano huo alipokuwa akiwahutubia wananchi.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadick akiteta jambo na Mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Mh. Jerry Silaa.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimwaga sera zake wakati akinadi ilani ya uchaguzi ya CCM katika mkutano wa kampeni jimbo la Ukonga.

Nani kakwambia vijana hawaipendi CCM angalia utulivu wa vijana hawa walipokuwa wakimsilikiza Tingatinga Dk. John Pombe Magufuli Ukonga leo.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Mh. Jerry Silaa.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Madabida mgombea wa viti maalum mkoa wa Dar es salaam huku Mwenyekiti wa CCM mkoa huo NDugu Ramadhan Madabida akifurahia.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano huo.

Wananchi wa mitaa ya Jimbo la Ukonga wakipiga Push up mbele ya Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akizungumza nao alipokuwa akielekea viwanja vya mkutano maeneo ya Moshi Bar Ukonga.

Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Kisarawe Mh. Seleman Said Jafo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Kisarawe.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo.

Mdau Michuzi Junior akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli

Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano huo mjini Kisarawe.

Ni lazima umuone Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli mwanangu.

SHARE