Home Audio Mgombea udiwani aahidi kununua chopa kwa ajili wa wajawazito

Mgombea udiwani aahidi kununua chopa kwa ajili wa wajawazito

SHARE
http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/05/chopa.jpg

Zikiwa
zimebaki siku 13 tu kufika siku ya kupiga kura, kampeni zinaendelea
kushika kasi huku wagombea wa nafasi mbalimbali wakitumia kila mbinu
kuhakikisha wanaongeza ushawishi kwa wananchi ili kujihakikishia
ushindi.

Katika
hali ambayo imeonyesha kuwafurahisha wakazi wa kata ya Mnyanjani,
mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Suleiman
Khafidh amesema iwapo watamchagua atanunua helkopita kwa ajili ya
kubebea wajawazito na wazee kuwapeleka hospitali.
Alizungumza hivi karibuni katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Mnyanjani, Khafidh alisisitiza
wajawazito na wazee wanapata kero kubwa sana kufikia huduma za afya
ambapo baadhi yao wanajifungulia njiani kutokana na ubovu wa barabara
hivyo wakimchangua yeye tatizo hilo litakuwa historia, Atanunua
helkopita . Kauli hiyo ilionekana kuwafurahisha sana wananchi ambao
walimshangilia hivyo wakimtaka aitekeleze haraka.’’ Ndugu zangu mimi
ndiye mgombea mdogo kuliko wote nitatekeleza” alisema Suleiman
SHARE