Home Audio KISA UCHAGUZI…MADEREVA DALADALA DAR WALIA KUKOSA ABIRIA !

KISA UCHAGUZI…MADEREVA DALADALA DAR WALIA KUKOSA ABIRIA !

SHARE
Barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni-Biafra hali ilivyoonekana, watu wachache barabarani.

Watu wakionekana wachache tofauti na siku za kawaida. Hapa ni maeneo ya Kinondoni-Studio.
Barabara ya Morogoro eneo la Magomeni-Mwembechai ikionekana kutokuwa na watu au foleni kama ilivyozoeleka.

Eneo maarufu la Manzese-Darajani lilivyoonekana kufuatia uchaguzi tofauti na siku nyingine.

BAADHI ya madereva wa daladala jijini Dar wamelia kukosa abiria katika vituo vyao kutokana na uchaguzi wa madiwani, wabunge na urais ambapo watu wamekuwa wakisubiria matokeo.

Akizungumza na Mtandao wa GPL, mmoja wa madereva daladala aliyejitambulisha kwa jina moja la Suleiman anayesafirisha abiria kutoka Kituo cha Makumbusho na Mabibo amesema kuwa suala la uchaguzi limechangia wao kukosa abiria kutokana na watu wengi kutokwenda katika shughuli zao za kawaida.

“ Ebwana eee…yaani mtaani katika vituo vyetu tunavyopita hakuna abiria kabisa, suala la uchaguzi limeharibu kabisa biashara zetu,” alisema Suleiman akiungwa mkono na madereva wengine waliokuwa wakisubiria abiria kwenye Kituo cha Kinondoni-Studio. 

LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

SHARE