Home Audio Kikwete: Magufuli Ameshashinda, Bado Kuapishwa tu!!

Kikwete: Magufuli Ameshashinda, Bado Kuapishwa tu!!

SHARE

MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema tayari
mgombea urais wa chama hicho, Dk John Magufuli ameshashinda uchaguzi.

Amesema
hatua hiyo inatokana na sababu mbalimbali, lakini kubwa ni kwa mgombea
huyo kuzunguka nchi nzima na kuwahakikishia wananchi, bila kupepesa
macho, kwamba atapambana na rushwa na ufisadi huku wagombea wengine
wakisita kuzungumzia rushwa.

Katika
hatua nyingine, Dk Magufuli ametaja mambo manne atakayoanza nayo kuwa
ni umasikini, tatizo la ajira, mapambano dhidi ya rushwa na amani.

Pia,
aliwapa pole Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais
Kikwete kwamba katika utawala wao, bila kujua waliwaweka madarakani
mafisadi waliochelewesha maendeleo ya serikali zao.

Rais
Kikwete na Magufuli waliyasema hayo katika viwanja vya Jangwani, Dar es
Salaam jana wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mkuu kwa
Jiji hilo. Mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya watu na viongozi
mbalimbali wa CCM, Serikali na viongozi kutoka nje ya nchi.

Akimnadi
Dk Magufuli, Rais Kikwete alisema kutokana na kampeni alizozifanya nchi
nzima kwa gari, ni wazi kwamba mgombea huyo wa CCM ameshashinda
uchaguzi huo. Alisema wagombea wengine pamoja na kutumia helikopta,
lakini walishindwa kuzungumza majukwaani.

Alisema
pamoja na kuelezea mambo mbalimbali atakayowafanyia wananchi kwa kila
kundi, amekuwa mgombea pekee ambaye bila kupepesa macho amezungumza
waziwazi azma yake ya kupambana na rushwa na kuwakabili mafisadi ili
kuwatokomeza.

Alisema
tangu kuanza kwa kampeni zake Dk Magufuli ametembea kilometa 46,000
nchi nzima, umbali aliosema umemwezesha kukutana na wananchi wengi
vijijini. Alisema wakati yeye alipofanya kampeni mwaka 2005, alitembea
kilometa 32,000 kwa gari na kuwa hoi katika siku za mwisho za kampeni.

Alisema
pamoja na kuzungumzia rushwa, Dk Magufuli amezungumzia masuala mengine
mengi kama kupambana na umasikini, ajira, amani, mikopo kwa wakulima,
wavuvi na wafugaji, kushusha kodi kwa wafanyakazi, kufuta ada kuanzia
darasa la kwanza hadi kidato na nne, lakini pia kuanzisha viwanda.

Akirejea
taratibu zilizomwezesha Dk Magufuli kuteuliwa na chama hicho kugombea
urais, Rais Kikwete alisema hakuna jipya lililofanyika katika kumpata
mgombea huyo, badala yake ni taratibu zile zile zilizotumika mwaka 1995
kumpata Rais mstaafu Mkapa na mwaka 2005 alipoteuliwa yeye.


“Ni
taratibu zilezile ndizo zilizotumika, hakuna utaratibu mpya. Katiba ya
CCM inasema Kamati Kuu itapitisha majina ya watu wasiozidi watano na
kuyapeleka kwenye Halmashauri Kuu, inaweza kuwa chini ya hapo lakini
wasiozidi watano,”
alisema Rais Kikwete akimjibu Kingunge Ngombale- Mwiru anayedai kupitia majukwaa ya Ukawa kuwa CCM ilikiuka taratibu.

Akizungumzia
mikopo kwa wanafunzi, Rais Kikwete alisema ni faraja kuona kuwa Dk
Magufuli amepania kukabiliana na usumbufu wanaokumbana nao.

Alisema
wakati alipoingia madarakani mwaka 2005, alikuta Sh bilioni 40 tu
zikitolewa kwa wanafunzi, huku wanafunzi 16,000 tu wakinufaika, na sasa
Sh bilioni 350 zinatumika na kuwanufaisha wanafunzi 98,000.
Chanzo:Mpekuzi blog
SHARE