Home Audio FUNDI MBARONI UBAKAJI WA DENTI!

FUNDI MBARONI UBAKAJI WA DENTI!

SHARE

Mtuhumiwa huyo akiwa chini ya ulinzi.

LAANA! Njemba mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, anayejishughulisha na ujenzi wa nyumba, mwishoni mwa wiki alinaswa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mdogo wa kike (10) katika nyumba aliyokuwa akiijenga maeneo ya Kichangani mkoani hapa, Risasi Mchanganyiko linakujuza. 

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa, alikuwa akienda kununua maziwa mtaa wa pili, ndipo jamaa huyo alipomuita ndani ya nyumba hiyo na kufanikiwa kumbaka akiwa amemziba mdomo, kumzuia asipige kelele.

….Akitolewa katika kituo cha polisi.
Inadaiwa kuwa baada ya kumaliza kufanya kitendo hicho, mtoto huyo
aliendelea na safari yake ya kununua maziwa, lakini aliporejea nyumbani,
mama yake aligundua hali isiyo ya kawaida hivyo kumuuliza nini
kilimsibu.
“Ndipo huyo binti akamwambia mama yake kuwa alipokuwa akienda kununua
maziwa, aliitwa na huyo fundi na kufanyiwa kitendo kibaya, jambo ambalo
lilimfanya mama huyo kumchukua mwanaye na kumpeleka polisi, ambako
walishauriwa kwenda hospitalini kwanza na huko ikathibitika kuwa kweli
alibakwa,” alisema shuhuda huyo.
….Akipakizwa kwenye gari.

Baada ya vipimo hivyo, mama na mwanaye walirejea tena polisi ambao baada
ya kuelezwa hivyo, waliongozana na watu hao hadi eneo la tukio ambapo
walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa
Morogoro ili kusubiri mchakato wa kupelekwa mahakamani.
SHARE