Home Audio Familia ya Mwanamuziki Diamond Yammwaga Rasmi Zari..Sababu Hizi Hapa

Familia ya Mwanamuziki Diamond Yammwaga Rasmi Zari..Sababu Hizi Hapa

SHARE

THE game is over! Sasa ni wazi kuwa familia ya staa mkubwa wa muziki wa
kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnamz’ imemtema rasmi mzazi
mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile wanachodai ….
“Tumechoshwa na uzungu wake”, Risasi Mchanganyiko linaweza kuandika.

Chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti hili kuwa kina
taarifa kuwa mama Latiffa ‘Tiffah’ hatarejea tena nchini kutokana na
kushindwana na wanafamilia, kwani wanaendekeza uswahili, kitu ambacho
yeye hakiwezi.

“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea mambo ya
kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao
wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo
hicho.

FAMILIA YA DIAMOND HII HAPA

Ili kujua ukweli wa maelezo hayo, mwandishi wetu alimtafuta mama mzazi
wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kupitia simu yake ya mkononi, na
alipoulizwa, alihamaki na kuanza kufoka, akidai hataki kuingiliwa mambo
yake ya ndani na kwamba kama kuna mtu anataka kujua zaidi amfuate Zari
huko kwao (South Afrika).

“Hata kama ni kweli, mimi na huyo sijui Zari wenu tumegombana wewe
yanakuhusu nini? sipendi kuingiliwa kwenye mambo ya familia yangu,
ninachojua ni kwamba hayupo hapa na maisha yanaendelea,” alisema Mama
Diamond na kukaa kimya huku simu ikiwa hewani.

Wakati simu ikiwa hewani, ghafla sauti ya kiume ilisikika na
kujitambulisha kwa jina la Anko Salum, aliyemtaka mwandishi kuachana na
habari hizo, kwani ni za ndani na zitamalizwa na wenyewe kama familia.

Wakati mwandishi wetu akiendelea kuzungumza na Anko Salum, ghafla tena
sauti nyembamba na kali masikioni ilisikika na mwanahabari wetu
akaibaini kuwa ni ya Esma, ambaye ni dada wa Diamond.

“Mbona mnatufuatilia sana jamani? Nani anafuatilia mambo yenu? Nafasi ya
Zari imefika mwisho, tunamkaribisha mwingine yeyote, kama kuna msichana
mrembo unamjua, tuletee nyumba yetu ni kubwa sana, na sisi tunaruhusiwa
kuoa hata wanawake wanne, Zari ameishia hapo, tena hatujagombana naye,
lakini tumechoshwa na uzungu wake, awamu hii tunahitaji mswahili
mwenzetu.

“Zari ameenda kwao, kulea watoto wake na kuangalia ustaarabu mwingine,
tunamtakia kila la kheri, lakini hatuna ugomvi naye kabisa,” alisema
Esma.Jitihada za kumpata Diamond hazikuzaa matunda kutokana na namba
yake ya mkononi kutokuwa hewani kila alipopigiwa, hata hivyo jitihada
zaidi zinaendelea kumtafuta.

Source:Global Publishers

SHARE