Home Audio Faiza Ally atangaza kuwa mjamzito kutoka kwa mpenzi wake mpya, Hamtaki tena...

Faiza Ally atangaza kuwa mjamzito kutoka kwa mpenzi wake mpya, Hamtaki tena Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’

SHARE
Muongozaji wa filamu hapa nchini Faiza Ally ambaye alikuwa mpenzi wa Mh Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr II au Sugu amefunguka kuwa na mpenzi mwingine mbali na Sugu kama ilivyo dhaniwa siku za hivi karibuni kuwa anataka kurudiana naye.

Faiza alizungumza hayo usiku wa kuamkia leo kwenye show ya Friday Night Live inayorushwa na EATV pale alipo ulizwa kuhusiana na post aliyo iweka Instagram na kuonyesha kuwa anataka kurudiana na Mh Mbilinyi.


Ndipo alipofunguka kuwa kwa sasa anampenzi mwingine na wala hayupo tayari kuwa na Sugu kwa sasa maana hata wakati alipo kuwa mahakamani kuhusiana na kesi yake ya muachilia mtoto wake akae na baba yake huyo tayari Sugu alishaweka bayana kuwa na mpenzi mwingine ambaye angeweza kumlea mtoto wao.

Faiza aliieleza FNL kuwa mbali na kuwa na mpenzi mwingine,
Anadhani kuwa inawezekana pia akawa na ujauzito kutoka kwa mpenzi wake
huyo wa sasa, Na kama hana basi angependa kuupata ujauzito kutoka kwa
jamaa wake ambaye sio wa hapa Bongo bali wa ughaibuni.

LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                        

SHARE