Home Audio Dk John Magufuli Ammwagia sifa Dk Slaa Karatu

Dk John Magufuli Ammwagia sifa Dk Slaa Karatu

SHARE

Mgombea
urais wa CCM, Dk John Magufuli jana aliwahutubia mamia ya wakazi wa
Karatu na kummwagia sifa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo na Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa ni kiongozi mwadilifu.

Akihutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mbowe mjini Karatu, Dk
Magufuli alisema Dk Slaa ni kiongozi wa upinzani ambaye alikuwa
mwadilifu akitetea masilahi ya umma.
Alisema kama angekuwa anagombea katika jimbo hilo, angemwombea kura kwani ni mtu safi bila kujali chama chake.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu wa Karatu, Dk Magufuli aliwataka kumuunga mkono Dk Slaa kwa uamuzi ambao amechukua.
Dk
Slaa, alitangaza hivi karibuni kuachana na siasa za vyama na kujitoa
Chadema baada ya kutoridhishwa na kujiunga kwa Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa katika chama hicho.
SHARE