Home Audio DIAMOND PLATNUM APOKELEWA KIFALME JIJINI DAR

DIAMOND PLATNUM APOKELEWA KIFALME JIJINI DAR

SHARE
MWANAMUZIKI nguli wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ leo
amepokelewa kwa shangwe na mamia ya mashabiki wake waliohudhuria katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Diamond ametua nchini akitokea Marekani alipokwenda kwa ajili ya zoezi
la utoaji tuzo za Afrimma ambapo alitwaa jumla ya tuzo tatu.
Baada ya mapokezi hayo Diamond akiwa na msafara wa mashabiki wake
walielekea Escape One, Mikocheni kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari
pamoja na kupiga picha za pamoja na mashabiki wake.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini
Marekani alipotwaa tuzo tatu za Afrimma.
Diamond akiwa na tuzo zake akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) muda mfupi baada ya kutua uwanja wa ndege.
Diamond akianza safari ya kuelekea Escape One kutoka uwanjani hapo.
Akiwa barabarani kuelekea Escape One.
Bodaboda wakiongoza msafara wa Diamond kuelekea Escape One.
Diamond akizidi kukatiza mitaa mbalimbali ya jiji la Dar.
Mashabiki wakia katika msafara wa Diamond.
Diamond akiongea na mashabiki wake njiani wakati akielekea Escape One.

(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)
SHARE