Home Audio
SHARE
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM), kimejitangazia ushindi wa majimbo 176 kati ya 264
nchini ambayo yamejumlishwa katika matokeo yaliyobandikwa katika vituo
mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Januari
Makamba, alisema chama hicho kimefanikiwa kukomboa majimbo 12 yaliyokuwa
yakishikiliwa na vyama vya upinzani.
“Kwa kuwa matokeo yamebandikwa hadharani na yamesainiwa na mawakala na
wakapewa nakala, CCM hadi sasa tumepata majimbo 176 kati ya 264 na 12
kati ya hayo tuliyoongoza yalikuwa chini ya upinzani katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita,” alisema.
Katika hatua nyingine, Makamba aliwataka wana- CCM kupuuza matokeo
yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii, na kwamba matokeo rasmi
yatatangzwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
“Tunawaomba watu wayapuuze matokeo hayo kwa sababu tumebaini bahati
mbaya wenzetu wanatoa matokeo ya uongo mapema ili tume ikitoa yaliyo
rasmi waseme wameibiwa kura ili kutafuta kisingizio cha kuingia mitaani
na kufanya vurugu.
“Pia tumebaini jitihada na nguvu kubwa za wapinzani wetu kupeleka kilio
chao kwa waandishi wa habari wa nje ya nchi pamoja na mataifa ya nje kwa
ujumla, wameajiri magwiji wa propaganda kutoka nje kwa fedha nyingi ili
kujenga taswira kwenye jumuiya ya kimataifa kwamba Tanzania ni kama
nchi nyingine barani Afrika ambako hakuna ustaarabu wala utaratibu wa
kidemokrasia na Serikali hukandamiza watu wake,” alisema.
Alisema mkakati wa wapinzani ni kuitaka jumuiya ya kimataifa itumie
nguvu yake ya misaada kwa Tanzania kulazimisha matokeo ambayo hayatokani
na utashi wa wananchi, na kwamba CCM haiko tayari kulikubali jambo
hilo.
Akizungumza suala la Zanzibar ambako mgombea urais wa Chama cha Wananchi
(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amejitangazia matokeo kuwa ameshinda,
alisema CCM wanayapuuza kwani hayajatangazwa na mamlaka husika.
“CCM tunayapuuza na tunaona huu ni mzaha na ndiyo maana tunawasisitiza
wananchi wayapuuze kwa sababu anayestahili kutangaza ni Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC).
“Tunahimiza utulivu kwa wafuasi wetu na wananchi kwa ujumla na waziachie
mamlaka husika zifanye kazi yake, hasa katika kipindi hiki kigumu cha
kupokea matokeo na kazi ya tume ni kuyatangaza,” alisema.
Alisema mamlaka za mawasiliano zikumbuke wajibu wake katika kusimamia
mitandao ya kijamii na kwamba wananchi wafuate kurasa sahihi za vyombo
vya habari kupata taarifa sahihi za matokeo.
Makamba alisema changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha uchaguzi
kamwe haziwezi kubadili utashi wa wapigakura, na kwamba haziwezi kubeba
chama chochote cha siasa.
“Cha msingi wananchi wawe watulivu kwa sababu tunaingia katika kipindi kigumu zaidi cha kupokea matokeo,” alisema.

– See more at: http://mtanzaniatz.blogspot.com/2015/10/ccm-tumeshinda-majimbo-176-wananchi.html#sthash.5g8ik9em.dpuf