Home Audio BREAKING NEWS! Matokeo ya uchaguzi Zanzibar yafutwa

BREAKING NEWS! Matokeo ya uchaguzi Zanzibar yafutwa

SHARE

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na kuwa na dosari nyingi ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru na wahaki.Mwenyekiti wa ZEC amewaambia waandishi wa habari mchana huu kuwa amechukua maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa uchaguzi ulighubikwa na dosari nyingi.
“Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa….

“Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza”! – Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

CHANZO NI BBC SWAHILI

LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA CHINI                                                                                     

SHARE