Home Audio Bayern Munich yaiwekea ngumu Man Utd juu ya uhamisho wa Muller

Bayern Munich yaiwekea ngumu Man Utd juu ya uhamisho wa Muller

SHARE

Thomas Muller amekuwa katika rada za Man utd tangu mwanzo wa msimu mpya wa 2015/16.Kwa mujibu wa CEO wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge, United imekuwa ikimtumia ujumbe wa barua pepe ya usajili wa kiungo mshambuliaji Thomas Muller na bila
kupepesa macho Rummenigge amewajibu United waache kumtumia ujumbe wowote unaohusiana na biashara ya Muller.
Rummenigge, akiongea baada ya ushindi aa Bayern dhidi ya Dortmund, amesema mchezaji huyo wa Ujerumani ambaye alifunga magoli mawili vs BVB, hauzwi.

Mkurugenzi wa klabu ya Bayern Munich,Karl-Heinz Rummenigge.
‘Hii sio bank, hii ni timu ya soka, na ndio maana hatufikirii hata kidogo kumuuza, niliwaambia rafiki zangu wa Manchester United sitoweza kuifunga akaunti yangu ya email ila mnaweza kuacha kunitumia ujumbe wowote unaohusiana na biashara ya kumnunua Muller.’
Hii sio mara ya kwanza kwa Rummenigge kuikatisha tamaa United juu ya usajili wa Muller.
Alipoulizwa juu ya upatikanaji wa Muller wakati wa dirisha la kiangazi alisema: ‘Kuna baadhi ya wachezaji hawana price tag, tutakuwa vichaa kumuuza Muller.’

SHARE