Home Audio Ajali mbaya: vijana 6 wa JKT Bulombora Kigoma wapoteza maisha, 21 wajeruhiwa

Ajali mbaya: vijana 6 wa JKT Bulombora Kigoma wapoteza maisha, 21 wajeruhiwa

SHARE
VIJANA
sita waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha
821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21
kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jana.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. 
“Ni
kweli leo majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa
JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21. “Wengine
wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma”alisema Dkt
Fadhili.
Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini. 
“Bado
tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza
maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana
fahamu”, alisema. 
Naye
kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema chanzo
cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na
kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka. 
Alisema
ajali hiyo imetokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori
hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba
makreti ya soda na unga.
SHARE