Home Audio SUMAYE: Walioficha fedha nje watazirudisha; Magufuli haiingii Ikulu 2015

SUMAYE: Walioficha fedha nje watazirudisha; Magufuli haiingii Ikulu 2015

SHARE
Fredrick Sumaye

Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye,  
amesema kama Lowassa atafanikiwa kuingia madarakani Watanzania
walioficha fedha nje ya nchi watazirudisha.Sumaye alitoa kauli
 hiyo
jana alipohutubia mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Laini Polisi mjini
Nzega, Mkoa wa Tabora.

Kwa mujibu wa Sumaye, fedha hizo ambazo
Serikali ya CCM imeshindwa kuzirudisha zitatakiwa kurudi kwa sababu ni
mali ya Watanzania.

“Jana (juzi) mmemsikia Magufuli (Mgombea
urais wa CCM, Dk. John Magufuli), akisema atakapoingia madarakani
atarudisha mashamba ya wananchi yaliyoporwa.

“Kwanza kabisa namwambia Magufuli kwamba
Ikulu haingii, lakini sisi tutakapoingia madarakani  tutahakikisha
walioiba fedha za Watanzania na kuzificha huko Ulaya au Uswisi
wanazirudisha,” alisema Sumaye.

Sumaye pia alizungumzia suala la rushwa
nchini na kusema kama CCM wangekuwa waungwana wasingemsimamisha mtu
yeyote kugombea urais kwa sababu wameshindwa kuwaletea maisha bora
Watanzania.

“Magufuli anasema akiingia madarakani
atakomesha rushwa sasa kama ana uwezo huo kwa nini ameshindwa kuikomesha
wakati na yeye ni waziri katika Serikali iliyokithiri kwa rushwa?

“Magufuli anasema akiingia madarakani
atakuza uchumi, kama kweli ana uwezo wa kukuza uchumi kwa nini
ameshindwa kuukuza kupitia Serikali ya CCM ambayo yeye ni waziri?

“Magufuli hana lolote, msimchague kwa
sababu ameshiriki kununua feri mbovu inayotoka Bagamoyo  kwenda Dar es
Salaam,” alisema Sumaye.

Katika maelezo yake, Sumaye alizungumzia
pia taarifa za viongozi wa CCM wanaodaiwa kuwatisha wananchi
wasimchague Lowassa kwa kisingizio kwamba nchi itaingia katika vita kama
ilivyotokea Libya na katika nchi nyingine za Afrika Kaskazini.

Sumaye alisema hakuna vita itakayotokea
 wapinzani watakapoingia madarakani na kwamba vita hiyo itatokea kama
Serikali ya CCM haitataka kuondoka madarakani.

SHARE