Home Audio SITOI AHADI AMBAYO HAITEKELEZEKI” ASEMA DKT MAGUFULI

SITOI AHADI AMBAYO HAITEKELEZEKI” ASEMA DKT MAGUFULI

SHARE


MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake atahakikisha baadhi ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa marais waliomtangulia,amesema
kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya wananchi ili awe Rais hatakuwa tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni dhambi na kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.

Akizungumza kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais, Dk.Magufuli aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi waliomtangulia kuongoza nchi.

Alisema sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo marais ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na awamu ya nne.

“Iwapo nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza .Yupo mzee Ali Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete,Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman Abeid Karume.

“Huu ndio utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa ushauri katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania.Najua msimamo wangu na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu.Narudia tena kwangu mimi ni kazi tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili nifikie malengo yangu,”alisema.

Alisema kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.

Dk.Magufuli ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara Mkoa wa Morogoro.

SHARE