Home Audio MAGUFULI ATINGISHA DODOMA MJINI MKUTANO WAKE WAFURIKA KULIKO KAWAIDA

MAGUFULI ATINGISHA DODOMA MJINI MKUTANO WAKE WAFURIKA KULIKO KAWAIDA

SHARE

 Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa
jamhuri tayari kuhutubia wakazi wa Dodoma mjini.

 Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa
Dodoma mjini waliofurika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya
uwanja wa Jamhuri mjini hapo.

 Waziri
Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akielezea umuhimu wa amani
katika Taifa letu na kusema kuna umuhimu wananchi kujifunza historia
kabla ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kwani itasaidia kutunza
na kuilinda misingi iliyowekwa na waasisi wa  Taifa hili.
Warioba
alimpongeza sana mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
kwa kuhubiri amani katika kila mkutano wake wa kampeni kitu ambacho
kinasaidia sana kuwakumbusha wananchi wa Tanzania kudumisha na kuitunza
amani kati yetu.

 Mgombea
Ubunge jimbo la Dodoma mjini akimuelezea Mgombea wa Urais wa CCM Dk.
John Pombe Magufuli changamoto mbali mbali za Dodoma mjini kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.

 Mgombea
ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony Mavunde akihutubia wakazi
wa Dodoma mjini mbele ya mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe
Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.

 Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Abdalla
Bulembo akihutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za
kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa
Jamhuri mjini hapo.

 Mgombea
wa Ubunge jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akicheza muziki wa
vijana wa Temeke mtindo maarufu unaojulikana kama mapanga shaa sambamba
na Chegge na Temba .

 Mtayarishaji
wa Muziki wa Kizazi kipya P Funky Majani akiwasalimu wakazi wa Dodoma
na kuwaambia kila mmoja wao ana jukumu la kumpigia kura mgombea wa Chama
Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.

 Ali
Kiba katikati akiimba na kucheza pamoja na wacheza show wake kwenye
mkutano wa kampeni za CCM uliofnyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma.

 Msanii Tunda Man akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 Wahamasishaji wakicheza wakati wa mkutano wa kampeni za CCM.

 Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto)akiwa
jukwaani pamoja na viongozi wengine ,Mawaziri Wakuu wastaafu Jaji
Joseph  Warioba, Mzee Samuel Malecela, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma
Adam Kimbisa na Mgombea Ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony
Mavunde.

Mgombea
Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akipiga push up kama
ishara ya kumuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe
Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma.
SHARE