Home Audio Defao Aonekana Akiwa ‘Mchovu’ Kenya Huku Sura yake Ikiporomoka kwa Sababu...

Defao Aonekana Akiwa ‘Mchovu’ Kenya Huku Sura yake Ikiporomoka kwa Sababu ya Mkorogo

SHARE
Defao Kulia
Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao baada ya
kutosikika kwa muda mrefu ameonekana huko Kenya, akiwa na muonekano
tofauti na alivyozoeleka kutokana na kupungua mwili kwa kiasi kikubwa,
na weupe wa ngozi yake ukitia mashaka.
Defao ambaye hata hivyo haijajulikana rasmi ni shughuli gani imempeleka
huko Kenya, kutokana na muonekano huo, hisia za wengi zimetafsiri
kuyumba kisanaa na kiafya kwa msanii huyo aliyewahi kuwa gumzo kwa sanaa
yake katika bara la Afrika na Ulaya.

Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na kupungua kwa
mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao ulifanya vizuri
sana katika miaka ya nyuma.

SHARE