Home Audio Pluijm apangua kikosi Yanga

Pluijm apangua kikosi Yanga

SHARE
BAADA
ya kutolewa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati
maarufu Kombe la Kagame, Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm
amefumua kikosi chake.
Yanga
walitolewa kwa mikwaju ya penalti 5-3 na Azam FC katika mchezo wa robo
fainali uliochezwa Julai 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja
na Yanga kushiriki michuano hiyo lakini inaonekana Pluijm hajapata
kikosi cha kwanza cha kudumu kutokana na kupangua kila wakati kikosi
hicho.
Pluijm
alionekana wazi kuanza kupangua kikosi chake katika mchezo wa robo
fainali na mabadiliko aliyoyafanya kwenye kikosi chake yameonyesha wazi
kwamba hadi sasa hakuna mchezaji mwenye uhakika wa kupata namba katika
kikosi chake.
Yanga
waliosajili makipa watatu katika michuano hiyo walikuwa wakiwabadilisha
kila mchezo Deogratias Munish ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’ hali
inayonyesha kwamba, Pluijm bado hajapata kikosi cha kwanza.
SHARE