Home Audio Mbowe: Slaa anapumzika, msiwe na hofu

Mbowe: Slaa anapumzika, msiwe na hofu

SHARE
 

Akizungumza na Radio one mda wa saa 4, Mwenyekiti wa
Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema Dr
Slaa hawezi kuhama chama hicho na hafikirii kamwe, kwa sasa anapumzika
kwa likizo ya wiki moja. 

 
Alipoulizwa kuhusu Slaa kutokubaliana na ujio Wa Lowassa amejibu kila
kitu tulikubaliana na Slaa mwenyewe aliunga mkono suala hilo.

Mbowe amesema wananchi na wanachadema kwa ujumla wasiwe na wasiwasi
kwani hiki chama ni makini na hakiwezi fanya maamuzi bila maridhiano na
akasisitiza kuwapuuza wanaoeneza habari kuwa Slaa amejiuzulu siasa.

Alipoulizwa mara ya mwisho kuwasiliana na Dr Slaa ni lini akajibu jana saa kumi na mbili jioni.

Alipoulizwa walizungumza nini akajibu anajua yeye na Slaa.

Walipomuuliza hasa mbona sisi tukimpigia hapatikani akajibu sijui lakini mimi nimewasiliana nae jana.

Chanzo: Radio one

SHARE