Home Audio Mauaji ya viongozi yazidi kuongezeka Burundi

Mauaji ya viongozi yazidi kuongezeka Burundi

SHARE
Ghasia za kisiasa zinaendelea nchini Burundi hata baada ya uchaguzi mkuu kufanyika
Maafisa nchini Burundi wanasema kiongozi mmoja wa chama tawala
nchini humo alishambuliwa na kuuwawa katika mji mkuu, Bujumbura. Huyu ni
kiongozi wa tatu kushambuliwa katika muda wa siku tatu.

Maafisa hao walieleza  Come Harerimana, rais wa chama cha CNDD-FDD
katika wilaya ya Kanyosha alikuwa akielekea ofisini akiwa nyuma ya
pikipiki wakati umati ulipomrushia mawe. Bwana Harerimana alivutwa
kutoka kwenye pikipiki na kupigwa  risasi.

Burundi hivi sasa inashuhudia ghasia mbaya za kisiasa tangu
kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005. Ghasia hizi
zilianza mwezi April wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwa
atawania muhula wa tatu madarakani hatua ambayo wapinzani wake na
mataifa ya magharibi walisema inakiuka katiba na mkataba wa amani wa
Arusha ambao ulipelekea kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Uchaguzi nchini Burundi

Uchaguzi nchini Burundi

Rais Nkurunziza alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa kiti cha
urais uliofanyika hapo Julai 21 kufuatia miezi kadhaa ya maandamano
mitaani na jaribio la mapinduzi lililoshindikana.
source SAUTI YA AMERIKA

SHARE