Home Audio K.K.K.T WAPATA ASKOFU MKUU MPYA WA KUONGOZA KANISA HILO NCHINI NI DK...

K.K.K.T WAPATA ASKOFU MKUU MPYA WA KUONGOZA KANISA HILO NCHINI NI DK FREDRICK SHOO

SHARE

MAASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemchagua Askofu Dk. FREDRICK SHOO kua mkuu mpya wa Kanisa hilo.

Uchaguzi huo uliofanyika jana kufuatia kumalizika kwa muda wa uongozi wa wa Askofu Mkuu wa KKKT Dk. Allex Malasusa.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Shoo alikua ni Askofu Mkuu wa Jimbo.la Kaskazini.
Askofu Mkuu Mteule, Dk. Shoo alizaliwa mwaka 1959 na kabla ya uchaguzi huo, alikuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo kwa miaka 10 kuanzia mwaka 2004.
Alibarikiwa kuwa Mchungaji Desemba 14 mwaka 1986 katika Usharika wa Lyamungo Kati. Kuanzia mwaka 1986 hadi 1988, alikuwa Mchungaji Kiongozi katika Usharika wa Mwika.
Alipata shahada ya uzamili na uzamivu nchini Ujerumani. Alikuwa Mkuu wa Chuo cha Biblia Mwika, mwaka 1995 hadi 2003. mtiwadawa Blog inatoa pongezi kwa Askofu Dk Shoo
SHARE