Home Audio Hatimaye Dr. Slaa Aonekana Baada ya Takribani Wiki Mbili Mafichoni

Hatimaye Dr. Slaa Aonekana Baada ya Takribani Wiki Mbili Mafichoni

SHARE
Mbunge mstaafu wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama
“Ndesa Pesa”, amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa
CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko
mapumzikoni, Dkt. Wilbrod Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.Ndesamburo alifuatana na makada wenzake wa chama hicho, baadhi yao ni
Meya wa Manispaa ya Moshi ambaye pia ni mgombea ubunge (mtarajiwa), wa
jimbo hilo, Japhary Michael.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya nini wamezungumza, ingawa makada
hao wa CHADEMA walikuwa jijini kuhudhuria mkutano mkuu maalum wa chama
hicho uliomteua Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa, kuwa mgombea
wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya mwavuli wa
muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA. Mgombea
mwenza aliyeteuliwa ni Mhe. Juma Duni Haji.

SHARE