Home Audio CCM YAKANUSHA UZUSHI WA MITANDAO YA KIJAMII

CCM YAKANUSHA UZUSHI WA MITANDAO YA KIJAMII

SHARE
2
Ndugu
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akitolea ufafanuzi
mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari wakati akizungumza nao kwenye
mkutano uliofanyika CCM Lumumba jijini Dar es salaam.
1
 

Ndugu
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akielekea kwenye ukumbi
wa mkutano kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari, huku akiwa
ameshikilia kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa
jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Ilani
hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 25 Agosti ndiyo itakayotumika kwa
kipindi cha miaka 5 ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa
ridhaa na wananchi kuongoza nchi kupitia mgombea wake wa Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, katika
uchaguzi mkuu ujao wa rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu kote nchini Tanzania.

Nape Nnauye amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao
ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dr. John Pombe
Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na
kila kijiji shilingi milioni 50 “Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani
ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo
hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM “.

Amefafanua
na kuongeza kuwa “Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza
kampeni mapema wakati hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na
taratibu za uchaguzi”. Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya
CCM Ofisi ndogo Lumumba leo.
3
Ndugu
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akiionyesha ilani ya
uchaguzi iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.
5
Hii ndiyo Ilani yenyewe.
6
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
7
Baadhi ya wapiga picha vyombo mbalimbali vya habari wakichukua matukio katika mkutano huo.
SHARE