Home Audio BODI YA MIKOPO YAWATAKA WAOMBAJI MIKOPO KUREKEBISHA TAARIFA ZAO

BODI YA MIKOPO YAWATAKA WAOMBAJI MIKOPO KUREKEBISHA TAARIFA ZAO

SHARE
BODI
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya
waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi
zimegundulika kuwa na upungufu na kuwataka kufanya marekebisho kabla au
ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo leo (Ijumaa, Agosti 28,
2015), jumla ya fomu za waombaji wa mikopo 7,788 kati ya 68,445
zilizopokelewa na kuhakikiwa zimegundulika kuwa fomu zina upungufu na
kuwataka waombaji kusoma majina yao katika tovuti ya Bodi 
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw.
George Nyatega, (Pichani) waombaji ambao fomu zao zimegundulika kuwa na
upungufu wanatakiwa kurekebisha kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba
mwaka huu (2015).
“Baada
ya kusitisha uombaji wa mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo
2015/2016, Bodi ilianza kufanya uchambuzi wa maombi yote yaliyopokelewa
na kugundua kuwa maombi 7,788 ya mikopo yanakosa taarifa muhimu,”
inasomeka taarifa hiyo.

  

Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, taarifa muhimu zinazokosekana ni pamoja na
sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na
picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na
wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama maelekezo yanavyotaka.
“Bodi
inawataka waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi zimegundulika
kuwa upungufu, kufika wao wenyewe katika ofisi za Bodi zilizopo Mwenge
jijini Dar es Salaam ili kufanya marekebisho katika fomu hizo,”
imesisitiza taarifa hiyo na kuongeza kuwa majina waombaji wanaotakiwa
kufika katika ofisi za Bodi yanapatikana katika tovuti ya Bodi
(www.heslb.go.tz).
Aidha,
Bodi ya Mikopo imewakumbusha waombaji wa mikopo kuwa waangalifu na
kuchukua tahadhari dhidi watu wasio waaminifu ambao wanaweza kutumia
zoezi hilo kuwadai fedha.
HESLB
ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi
mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa
wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

 Aidha,
jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa
kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati
Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

SHARE