Home Audio Zitto Kabwe Awataja Walioficha Mabilioni ya Fedha Uswisi

Zitto Kabwe Awataja Walioficha Mabilioni ya Fedha Uswisi

SHARE

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo katika viwanja  vya Mwembeyanga
jana amewataja watanzania walioficha mabilioni ya Fedha  katika Benki za
nje ya nchi.

 

Akizungumza na  wakazi wa jiji la Dar es salaam Zitto Kabwe amesema
 hivi sasa  uchumi wa nchi umeshikwa na watu wachache hususani
wafanyabiashara ambao pia wameshika siasa au kwa wao kushiriki kwenye
siasa moja kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea maslahi yao.

 

Ameongeza kuwa nchi ina Kansa ya Ufisadi ambapo  watu hutumia nafasi
zao za uongozi kujilimbikizia mali ikiwemo  viongozi walioshika madaraka
ya umma.

 

Mwezi Novemba mwaka 2012 Bunge lilipitisha Azimio namba Tisa
la Mwaka 2012 ambalo lilielekeza Serikali kufanya uchunguzi kuhusu
Watanzania na makampuni ya kitanzania waliotorosha na kuficha fedha
kwenye mabenki ughaibuni

 

Uchunguzi pia ulikuwa uhusike na Mali za Watanzania zilizopo nje ya
nchi katika juhudi za kuhakikisha kuwa fedha chafu na ufichwaji wake
vinakomeshwa. Bunge lilitoa muda wa miezi sita kwa Serikali kufanya
uchunguzi huo.

 

Mwaka mzima ulipita Serikali haikutoa maelezo yeyote na baada ya
kubanwa ndani ya Bunge Serikali ikaomba miezi sita zaidi. Hata hivyo
mpaka leo Serikali haijatoa kauli yeyote kuhusu taarifa hiyo ya
uchunguzi.

 

Ametolea mfano kuwa  taarifa ya Serikali ya kisiwa cha Jersey kilicho
chini ya himaya ya Uingereza inaonyesha kuwa Fedha na Mali za
Watanzania katika mabenki kisiwani humo ni paundi za Uingereza 440
milioni ambazo kwa bei ya sasa ni sawa na shilingi za kitanzania 1.4
trilioni.

 

Vile vile taarifa rasmi ya Benki Kuu ya Uswiss inaonesha kuwa
Watanzania wenye akaunti katika mabenki ya nchi hizo imefikia dola za
kimarekani 304 milioni kutoka dola 213 milioni mwaka 2012. Amesema  hana
takwimu kwa nchi nyingine duniani huku akisistiza kuwa fedha hizi
 zilizofichwa zaweza kuwa halali au haramu.

 

Amesisitiza kuwa Serikali imenyima haki hiyo kwa zaidi ya miaka
miwili na nusu sasa. Bunge la Kumi linavunjwa mnamo tarehe 9 Julai mwaka
huu na hakuna dalili yeyote ya Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi
ndani ya bunge kama ilivyoagizwa na Bunge.

 

Orodha hiyo amesema ali iwaslisha  kwa Gavana wa Benki Kuu,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwa ajili ya uchunguzi lakini Serikali mpaka sasa  haijatoa
taarifa licha ya kupewa kila aina ya ushirikiano.

 

“Nimeamua leo kuiweka orodha hii wazi kama shinikizo kwa Serikali
kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo.”Amesema
Zitto

 

Orodha hiyo ina majina 99 ya Watanzania au watu wenye mahusiano na
Tanzania ambao wana akaunti HSBC ya Uswiss. Jumla ya akiba katika
akaunti Benki hii pekee ni dola za kimarekani 114 milioni. 

 

Soma hapa kuona majina hayo……

SHARE