Home Audio TUZO YAMPA SHAVU BARAKAH DA PRINCE

TUZO YAMPA SHAVU BARAKAH DA PRINCE

SHARE
Msaniiwa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’
MSANII wa Bongo Fleva anayeshikilia Tuzo ya Mwanamuziki Bora
Chipukizi wa Mwaka (KTMA), Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ amelamba
shavu la kufanya kolabo za kimataifa na Jaguar kutoka Kenya pamoja na
Patoranking wa Nigeria.

Akifunguka na Centre Spread,
Barakah anayebamba na Ngoma ya Nivumilie aliyoshirikiana na Ruby kutoka
Jumba la Kuibua Vipaji (THT) alisema kuwa mbali na ujio huu alioutoa
hivi karibuni yupo mbioni kufanya kazi za kimataifa.

“Tuzo imenipa heshima kubwa mjini. Nipo
katika harakati za mwisho kufanya ngoma na Patoranking na baada ya hapo
menejimenti yangu itamalizana na Jaguar kisha mtanisikia nikiwa naye
katika ngoma moja,” alisema Barakah

SHARE