Home Audio NEC YAOMBWA KUONGEZA MUDA UANDIKISHAJI BVR DSM..DAR YAANZA KWA KUSUA SUA

NEC YAOMBWA KUONGEZA MUDA UANDIKISHAJI BVR DSM..DAR YAANZA KWA KUSUA SUA

SHARE

Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC),imetakiwa kuongeza muda wa Kujiandikisha
katika Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa jiji la Dar es Salaam
kutokana na wingi wa watu lakini ibadilishe baadhi ya sheria ili kila
mtu mwenye sifa apate haki ya kupiga kura

Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Said Miraji, akizungumza katika moja ya mikutano yao.

Akizungumza
katika Mkutano maalum wa chama cha ADC leo jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama hicho Said Miraji Abdallah amesema kuwa kuna watu
wenye sifa ambao wanakosa haki yao ya msingi wakiwemo wafungwa,
wagonjwa, na watanzania walio nje ya nchi ambao wanashindwa kupata haki
yako kutoka na mfumo wa sasa wa uandikishaji.
Bw. Miraji ameongeza
kuwa kuna watu ambao wanaweza kuachiwa magerezani wakati zoezi la
uandikishaji limeshapita hivyo litawafanya washindwe kushiriki katika
uchaguzi mkuu hivyo tume haina budi kuziangalia sheria zake upya.

Wakati
huo hou Aliyekuwa mbunge wa Wawi Zanzibar kupitia Chama cha WanancHi
(CUF) Hamad Rashid amejiunga rasmi na chama chake kipya cha ADC leo na
kukabidhiwa kadi namba moja.
Akiongea na waandishi wa habari Hamad
Rashid ametumia fursa hiyo kutangaza nia ya kuwania urais wa Zanzibar
ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwa tiketi ya chama hicho.

SHARE