Home Audio
SHARE
Nawashukuru Watanzania wote kwa ujumla wenu kwa
Ushirikiano,Imani,Upendo na Umoja mliouonesha kwangu wakati wote wa
Mchakato wa kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais kwa Chama changu cha
Mapinduzi.
Mchakato umemalizika salama,CCM ikiwa na Umoja na
mshikamano,Nampongeza sana kaka yangu J.P.Magufuli kwa kuteuliwa
kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu Mwaka
huu.Ninaimani kubwa kuwa wakati wa Mabadiliko kwa Vitendo umefika na
Taifa letu litapiga hatua kubwa zaidi ya hii kwenye Maendeleo.
Naomba tuendelee kushirikiana,kupigania Uchumi wa Taifa letu ufike kipato cha kati.
Kidumu Chama cha Mapinduzi
‪#‎UMOJANIUSHINDI‬
SHARE