Home Audio MZEE KINGUNGE ASEMA MCHAKATO ULIOTUMIKA KUMPATA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM...

MZEE KINGUNGE ASEMA MCHAKATO ULIOTUMIKA KUMPATA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM ULIKUWA BATILI

SHARE
Mwanasiasa mkongwe nchini na moja kati ya waasisi wa chama cha
mapinduzi mzee Kingunge Ngombaru Mwiru amesema mchakato wote uliotumika
katika kumpata mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM mwaka huu ulikuwa
batili.

Akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake jijini Dar es
Salaam, mwanasiasa huyo mkongwe hapa nchini kupitia chama tawala mzee
Kingunge Ngombaru Mwiru, amesema mchakato wa kumpata mgombea wa urais
ulikuwa batili kutokana na kamati ya maadili ambayo ni chombo cha kutoa
ushauri kufanya kazi ya kamati kuu ambayo ni kutoa maamuzi, hivyo kamati
ya maadili yenyewe ilishiriki kuvunja maadili.
Mwanasiasa huyo amesema kwa mujibu wa utaribu uliowekwa, wagombea
wote wangetakiwa kupita mbele ya kamati kuu na kujieleza na kuulizwa
maswali lakini haikufanyika hivyo, jambo ambalo si sawa huku akiongeza
kuwa kuna watu walikuwa na orodha ya watu wao kuhusu nafasi ya urais.
Kuhusu ndugu Edwaed Lowasa, Kingunge amesema hausiki katika kashfa
yeyote ya ufisadi kwa maana yeye aliwajibika kisiasa na si kwamba
alihusika katika kashfa ya Richmond.
SHARE