Home Audio MWEZI MTUKUFU,FUTARI YAZUA BALAA!

MWEZI MTUKUFU,FUTARI YAZUA BALAA!

SHARE
Akihojiwa baada ya kuminyiwa kichapo. 

 Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la
Asha, mkazi wa Mtaa wa Area Six, Kata ya Kichangani mkoani hapa ambaye
alikuwa kwenye swaumu ya Mfungo

wa Ramadhani, amejikuta akilazimika
kutengua swaumu na kumpa kichapo mwanaume aliyeiba futari na kiti chake
cha plastiki alichokuwa amekalia nje ya nyumba akipika futari hiyo.
Tukio
hilo la aina yake, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wakati
paparazi wetu anawasili kwenye eneo la tukio, alikuta kasheshe bin
tafrani ikiendelea. Mbali na mwanamke huyo, wananchi wenye ghadhabu nao
walikuwa wakimshikisha adabu mwanaume huyo huku wakidai ni mwizi.
Kwa mujibu wa chanzo, awali mwanamke huyo alikuwa nje ya nyumba yake akipika futari huku akiwa amekalia kiti hicho.

Akiomba kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.
“Ghafla
si akapata udhuru uliomlazimu aingie ndani. Akaacha futari ikitokota
jikoni. Amefanya yake kule ndani, akakumbuka ameacha futari jikoni,
akatoka.“Kufika! Kwanza akaona futari imepungua. Sasa ile anataka kukaa,
kiti nacho hakipo. Akashangaa.”
ATAFUTA KITI, AMWONA NACHO MTU
Chanzo
kiliendelea kudai kuwa, mwanamke huyo alianza kukisaka kiti chake
sehemu mbalimbali nyumbani hapo lakini bila mafanikio. Alipotupa macho
mbali na nyumbani, akamwona nacho huyu mwanaume amekibeba akitambaa
zake.
“Ndipo
mama bila kujali swaumu, akaingia ndani. Akachukua kirungu na sime na
kumfukuza mpaka akamkamata na kuanzia kumwangushia kipondo huku jamaa
akikitupa kile kiti kichakani kwa lengo la kupoteza ushahidi,” kilisema
chanzo hicho.
WANANCHI WAINGILIA KATI
Baadhi ya wananchi
wanaoaminika kuwa na hasira kali nao waliamua ‘kununua’ kesi hiyo ambapo
na wao walichukua silaha mbalimbali, yakiwemo mawe na kuanza kumbonda
mwanaume huyo mpaka damu chapachapa.
Anayedaiwa kuibiwa futari akimpiga kwa hasira.
BODABODA NUSURA WAMTOE UHAI, WAMVUNJA MGUU
Baadhi
ya madereva wa bodaboda walipomwona mwanaume huyo anazidi kuchakaa uso
kwa kipigo, badala ya kumwokoa, waliingilia kati na kutaka kumchoma moto
lakini wasamaria wema walipinga kitendo hicho na kumuokoa kwa
kumkimbizia kwenye Kituo cha Polisi cha Nanenane kilicho jirani na eneo
la tukio.
Hata hivyo, wakati akikimbizwa polisi, bodaboda hao
waliamua kumgonga na pikipiki kwa makusudi na mmoja wao alifanikiwa
kumvunja mguu.
MAMA MWENYE FUTARI
Alichonifanyia siyo haki kabisa, kama alikuwa na njaa, angeniambia, ningempakulia futari akala kuliko kuniibia.

SHARE