Home Audio Mwanamuziki JIDE Ala Bata China Huku Nyumba Yake Akipigwa Mnada Bongo

Mwanamuziki JIDE Ala Bata China Huku Nyumba Yake Akipigwa Mnada Bongo

SHARE
Deogratius Mongela na Chande Abdallah
GOOD time! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo wakati habari ya mjini ikiwa
ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada, staa wa Bongo Fleva, Judith
Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ yupo bize jijini Hong Kong, China akila
bata, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and
General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki
huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa
kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.

Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua
anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye
viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini
jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi
kutopatikana.

Wakati gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza
habari kuwa staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula
ujana’.“Kwa taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula
raha kama vipi fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,”
kilinyetisha chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.

Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda
liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na
posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.

Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa
kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.
GPL

SHARE