Home Audio MSHAMBULIAJI MPYA WA YANGA AMESEMA HAYA…

MSHAMBULIAJI MPYA WA YANGA AMESEMA HAYA…

SHARE
Donald NgomaMshambuliaji
mpya wa Yanga Donald Ngoma aliyesajiliwa akitokea FC Platinum ya
Zimbabwe, amesema amefurahi kujiunga na klabu hiyo ya Jangwani na
kuongeza kuwa, kucheza kwenye klabu hiyo sio kitu rahisi kwasababu timu
hiyo ni moja kati ya timu kubwa

barani Afrika na atajitahidi kufanya
kile ambacho mashabiki wanatarajia kutoka kwake.

“Nina furaha kujiunga na Yanga,
ni miongoni mwa klabu kubwa Afrika ina uongozi bora, mashabiki bora,
waalimu bora pia na kikosi bora. Hatukutegemea (yeye na Zuttah) kama
tungepata mapokezi kama haya kutoka kwa mashabiki tumeshangazwa sana na
jinsi mashabiki walivyo wengi na wanavyoipenda timu yao”, amesema Ngoma
Najua kuchezea klabu kubwa kama
hii kuna presha kubwa sana lakini naamini nitaishinda hiyo presha na
kufanya kile mashabiki wanachotarajia kutoka kwangu, siwezi ahidi
chochote zaidi ya kusema kazi yangu uwanjani ndio itatoa majibu”,
alisema Mzimbabwe huyo.
Donald Ngoma Dombo anaondoka leo
kurudi kwao kwa ajili ya kujiandaa rasmi ili kuja kuitumikia Yanga
ambapo atarudi Jumapili na siku ya Jumatatu ataanza mazoezi kujiandaa na
michuano ya Kagame.
SHARE