Home Audio WAALIMU WAMCHAMBUA MKE WA MAGUFULI

WAALIMU WAMCHAMBUA MKE WA MAGUFULI

SHARE

Mke wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Janeth Pombe.
K
UMEKUCHA! Siku chache baada ya Waziri wa
Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, mkewe, Janeth Pombe
amechambuliwa vilivyo na walimu wenzake, Amani lina kila kitu.

Juzi, Amani lilifika Shule ya Msingi
Mbuyuni, Oysterbay jijini Dar ambayo Janeth amekuwa akifundisha na
kufanikiwa kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo na walimu wengine.
MWALIMU MKUU AANZA
Akizungumza na gazeti hili, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Doroth Malecela (John Malecela anamwita baba mdogo) alisema:
“Kwetu sisi kama shule, tunajivunia kwa sababu hata mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mama Salma Kikwete alifundisha shule hii.
AOMBA MAGUFULI ASHINDE “Kama
John Magufuli atafanikiwa kuingia madarakani, taifa linatakiwa kujua
Mbuyuni ndiyo shule inayotoa marais wetu kupitia wake zao.
“Hivi sasa tunaomba uchaguzi uende vizuri, Magufuli ashinde ili naye
tumlee. Mbali na yote, lakini pia kuondoka Janeth kutatuachia pengo
kwetu maana tulikuwa naye kwa kipindi chote lakini ni wazi kwamba kama
mumewe atashinda urais, kisheria yeye Janeth hataweza kuendelea
kufundisha tena hapa,” alisema mkuu huyo wa shule.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dar.

MAISHA BINAFSI
Mwalimu Doroth alimchambua Janeth Pombe (jina analotumia) kuwa,
katika mazingira ya shuleni, mwalimu huyo aliishi kama walimu wengine na
si kama mke wa waziri kwa sababu hajikwezi. Hata mavazi yake ni simpo
tu.
“Kwanza Janeth ni mcheshi, lakini pia ni mpole na  mchapakazi. Ni mtu
wa kujichanganya na wengine kwenye shida na raha. Kwenye furaha
hakusita kuonesha uchangamfu wake hata kwa kucheza. Kila mmoja alipenda
uwepo wake,” alisema mwalimu huyo.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni ya jijini Dar.

MASOMO ANAYOFUNDISHA
“Hapa anafundisha wanafunzi wa darasa la tano  masomo ya Uraia, Historia na Jiografia.”
KUHUSU UCHELEWAJI
“Hapana, kwa kufuata taratibu za kazi na sheria za shule, mwalimu
Janeth alikuwa akifika mapema na kuanza majukumu yake bila kupoteza
muda.”
USAFIRI ANAOUTUMIA
“Amekuwa akiletwa kazini muda mwafaka na gari na dereva wake na muda
wa kutoka pia alifuatwa kwa gari bila aina yoyote ya mbwembwe.”

Kibao cha Shule ya Msingi Mbuyuni.

HAKUWA MTORO?
“Inapotokea ana udhuru wa kumfanya ashindwe kuhudhuria shuleni
amekuwa akitoa taarifa mapema kwa uongozi. Kifupi alikuwa mtiifu,
hakuringia cheo cha mumewe hata siku moja na haikuwa rahisi mtu kumjua
kuwa ni mke wa Waziri John Magufuli bila kuambiwa.
KUHUSU FAMILIA
“Pamoja na kuwa mume wake ni waziri,  watoto wao wote wamesoma katika
shule hii. Kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba na walikuwa
wakishirikiana na wanafunzi wenzao.
“Mtoto wao wa mwisho alimaliza hapa mwaka jana, sasa anasoma Shule ya
Sekondari ya Kata ya Oysterbay na kuna muda huwa anakuja  kutusalimia,”
alisema mwalimu mkuu huyo.
SHEMEJI UNATUACHAJE
“Kuna kipindi walimu tulisema JK unatuachaje shemeji yetu (kwa ajili
ya mama Salma), lakini alitujibu atakuja shemeji yenu mwingine. Kwa
usemi ule sasa tunaamini, shemeji yetu anaweza kupatikana tena.”
SIRI YA SHULE
Akieleza sababu inayoifanya shule yao kuibua wake wa marais (kama Magufuli atashinda) mwalimu huyo alisema:
“Hakuna siri kubwa, huku Oysterbay, Masaki ndo’ wanakoishi vigogo wa
serikali hivyo huwa ni rais wake zao kufundisha kwenye shule hii.”
ANAIJUA SIASA?
“Mama Magufuli yeye mara kwa mara husifia kazi yake ya ualimu, sikuwahi kumsikia akisema anapenda siasa hayupo huko kabisa.”
Waandishi: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani.

SHARE