Home Audio MBUNGE GODFREY MGIMWA ; NILIAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI WA KALENGA NIMEFANIKIWA KWA ASILIMIA...

MBUNGE GODFREY MGIMWA ; NILIAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI WA KALENGA NIMEFANIKIWA KWA ASILIMIA 99 NDANI YA MWAKA MMOJA PEKEE

SHARE
mbunge  Mgimwa akitimiza ahadi yake  ya bati 50 kwa kituo cha yatima  Tosamaganga
Mbunge Mgimwa katikati  akitazama nguzo  za umeme katika kata ya Mgama 

WAKATI  
wabunge wakiwa  mbioni kumaliza muda wao   mbunge wa   jimbo la 
Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema kuwa kwa  kipindi chake cha mwaka
mmoja kama  mbunge wa   jimbo hilo la Kalenga amesema anamshukuru Mungu
katika  safari yake ya  kuwatumikia wananchi  wa  jimbo la Kalenga kwa
kufanikisha  kutekeleza ahadi  zake kwa asilimia 99.9 ndani ya  mwaka
mmoja .

Huku 
akiwaomba  wananchi  wa  jimbo hilo la Kalenga  kuweza kumpima kwa
kazi  alizozifanya kwa mwaka  mmmoja na zile zilizofanywa na wabunge
waliotangulia katika  jimbo hilo na  wabunge  wa upinzani kwa  kipindi
cha miaka  mitano walioongoza majimbo yao.

Bw
Mgimwa  aliyasema  haya  jana   wakati akieleza  utekelezaji  wa ilani
ya  CCM na ahadi  mbali  mbali zilizoahidi  mbunge aliyetangulia
Marehemu Dr Wiliam Mgimwa kwa kila kata kati ya kata 13 za jimbo la
Kalenga .

Alisema 
kuwa katika  kata ya Kiwere ahadi  ambazo amezitekeleza ni pamoja na 
mradi wa umeme vijiji vya Mgera ,kitapilimwa,Mfyome ambao unaendelea pia
Mradi
wa Maji, Mfyome na kiwere unaendelea,Bati 80 shule ya msingi
Kiwere,Bati 50 Itagutwa,vikundi vya vicoba kata ya kirewe vimepewa Tsh
milioni 3,ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kiwere amechangia milioni
2 ujenzi wa bweni sekondari ya Kiwere amechangia Tsh milioni 1

kata 
ya Nzihi  katika shule ya Dintyus sekondari amechangia Tsh milioni
2,saruji
mifuko 100,Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Kidamali
na mifuko 50 ya saruji, Tsh 400,000 kwa timu ya daraja la tatu ngazi ya
Mkoa wakati  kata ya Ulanda Shule ya msingi Lukwambe Bati 100, ujenzi
wao kituo cha afya Mlangali mchango wa Tsh 250,000,mradi wa maji kijiji
cha Mwambao,kijiji cha Weru ,mradi wa umeme Kijiji cha Ibangamoyo
,Kibebe na Weru
Mchango wa Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara Shule ya sekondari Kalenga
Mbunge  Mgimwa alisema kwa kata ya Kalenga  kwa  shule ya  msingi amechangia Tsh 660,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo
vya wanafunzi,Bati 50 na mabelu ya nguo za yatima Tosamaganga vyote
vikiwa na thamani ya Tsh milioni 3.5 pia amechangia Tsh milioni 2
ujenzi wa maabara Sekondari ya Lipuli ,mifuko 50 ya Saruji,Vicoba kijiji
cha kalenga Tsh 500,000 pamoja na vifaa vya michezo kwa vijana.
Huku kata  ya Mseke katika  shule ya  msingi Ugwachanya Bati 60 , shule ya msingi Sadani Bati 60 na
saruji 50 na Tsh milioni 1, shule ya msingi Makota Bati 50 Mseke
sekondari Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,kikundi cha
Sliki Tanangozi Tsh 700,000
Mradi wa umeme kijiji cha Wenda unaendelea wakati kata  ya Luhota kwa  upande wa Shule
ya msingi Wangama Bati 50 na saruji 50, kikundi cha siliki Tagamenda
Tsh 500,000 na Luhota sekondari Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa
maabara

Alitaja 
kata  nyingine  ambazo amechangia  kuwa ni Magulilwa kwa shule ya
msingi Nega B Bati 100,kijiji cha Mranda Bati 80, mradi wa umeme
Nega B na Magulilwa unaendelea, shule ya msingi Ng’enza Saruji mifuko
50 ,Visiwa viwili vya maji na shule ya sekondari Muwana Tsh milioni 2
ujenzi wa maabara na kata ya Lyamgungwe Kijiji
cha Malagosi Bati 80 za ujenzi wa zahanati,kijiji cha Lupembelyasenga
saruji 50 , mradi wa umeme Wenda,Kikombwe,Ismila na maji kijiji cha
Kikombwe unaendelea
Kuchangia Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara shule ya sekondari Ismila

Pia kata ya  Mgama kwenye shule ya  msingi Mgama Bati 100
na Tsh milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, shule ya msingi
Ibumila Bati 50 na saruji 50 ,shule ya msingi Itwaga saruji 20, shule
ya msingi Luhato madawati 30 na mradi wa umeme kijiji cha Mgama
unaendelea na kata ya Ifunda amechangia
Shule
ya msingi Mibikimitali Bati 50, Shule ya msingi Udumuka saruji
100,kijiji cha Mfukulembe Bati 50 ,shule ya sekondari Lyandembela
milioni 2 ujenzi wa maabara na Shule ya sekondari Lyasa Tsh milioni 2


Bw 
Mgimwa alisema  kuwa kwa kata   Lumuli ,kijiji
cha Isupilo Bati Bati 50 ,kijiji cha Muwimbi Bati 80 ,Lumuli sekondari
Tsh milioni 2 ujenzi wa Maabara,mradi wa umeme Isupilo,Itengulinyi,mradi
wa maji Isupilo ,Itengulinyi na Lumuli inaendelea pia kivuko cha
barabara ya Itengulinyi – Magunga kimekamilika wakati kata ya Wasa
,Shule ya msingi Usengelendeti Bati 100,Mahanzi Bati 80,WASA sekondari
Tsh milioni 2 ujenzi wa maabara,mradi
wa umeme unaendelea

Alitaja  utekelezaji wa ahadi alioufanya pia kata  ya Maboga  katika Shule
ya msingi chamgogo Bati 50 , Shule ya msingi Kidilo bati 50, Shule ya
sekondari Kiponzero Milioni 2 ujenzi wa maabara , barabara ya Magunga –
Makota umekamilika,shule ya msingi Makombe saruji mifuko 50 pia mradi
wa umeme Kiponzero unaendelea.

Mbunge 
huyo  alisema  kuwa jimbo la Kalenga kuna jumla ya kata 13 ila sasa ni
kata 15 ambazo zimetokana na kata mpya na kuwa  kiasi cha zaidi ya  Tsh 
milioni 110 amepata  kuzitumia kutimiza ahadi  zake kwa kipindi chake
cha mwaka  mmoja pekee aliopata  kuwepo madakarani

Hata 
hivyo  alitaja ahadi ambazo bado  kuzitimiza na atazitimiza  wakati 
wowote kabla ya kumaliza  muda  wake  kuwa ni  ahadi ya Tsh milioni 1
kwa ajili ya Vicoba Ifunda  kibaoni ,bati 100 kwa ajili ya kuchangia
ujenzi shule ya wasichana Ifunda ,ahadi ya Tsh milioni 1  kwa ajili ya
ununuzi  wa vyombo vya muziki katika  Kanisa la Lutherani Ifunda kibaoni
na ahadi ya  mwisho ni ya bati 60 kwa ajili ya shule ya  sekondari
Lyandembela
Hivyo 
aliwataka  wananchi  wa  jimbo la Kalenga  kuendelea kuwa na imani 
zaidi kwani amefanikiwa  kutimiza ahadi zilizonyingi ambazo amepata 
kuzitoa kwa  muda wa  mwaka  mmoja  pekee  na kuwa  iwapo  watamchangua
tena basi  wawe  na imani ya   kupata maendeleo  makubwa  zaidi ya haya .

Naomba  wananchi  wa Kalenga  niwahakikishie  kuwa nitagombea  tena 
Ubunge kwa mwaka  huu  ili  niweze kupata miaka  yangu mitano ya 
kushirikiana nanyi katika  kuleta maendeleo “
SHARE