Home Audio MAWAZIRI WA MKAPA BASILI MRAMBA NA DANIEL YONA WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA...

MAWAZIRI WA MKAPA BASILI MRAMBA NA DANIEL YONA WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU KWA KUITIA HASARA SERIKALI

SHARE

Vilio
simanzi na majozi vimetawala katika viunga wa mahakama ya hakimu mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam pale jopo la majaji watatu walipothibitisha
pasipo na shaka kuwa Bw Basil Mramba na Bw Daniel Yona waliokuwa ni
mawaziri wa

serikali ya awamu ya pili wanapaswa kwenda jela kwa miaka
mitatu na kulipa faini ya shilingi milioni tano kwa makosa yanaowakabili
yakiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisasabisha serikali
hasara.


Katika
mahakama hiyo ndugu wawashtakiwa hao walionekana kutoyaamini yale
yanayotokea na wengine kujikuta wakitiririkwa na machozi ambapo wakati
hao wakiwa katika hali hiyo ndugu wa upande wa aliyekuwa katibu mkuu
wizara ya fedha Bw.Gray Mgonja ambaye na yeye alikuwa ni miongoni mwa
washtakiwa walijikuta wanapigwa na butwaa baada ya ndugu yao kuachiwa
huru na mahakama hiyo baada ya kutokutwa na hatia yoyote.

Bw.Mgonja
ambaye muda mwingi alionekna kusimama tuu bila ya kuzungumza chochote
alijikuta anaishia na maneno ya kukiambia kituo hiki pale alipotakiwa
kusema lolote zaidi ya kusema hayo yote amemwachia mungu na yamefanyika
kwa rehema za mungu.

Awali wakili wa serikali Tumaniel Kweka
amesema Bw Mramba amekutwa na makosa kumi na moja isipokuwa Yona ambaye
makosa yake ni pungufu ya hapa na kwamba watapaswa kulipa fidia ya
shilingi milioni tano kwa kosa la kumi na moja na kama watashindwa
kulipa watapaswa kwenda jela kwa mika mitatu ingwa bado watapaswa kwenda
jela miaka mitatu kwa makosa hayo mengine.

Kwa upande wakili
wa utetezi wamesema hawajaridhiswa na hukumu hiyo na hivyo watakata
rufaa ndani ya kipindi kifupi kijacho itakumbukwa kuwa washtakiwa hao
walifikishwa mahakamani hapo kwa kuwa walikuwa watumishi wa umma ambao
Oktoba 30 mwaka 2003 walikaidi ushahuri wa mamlaka ya mapato Tanzania
wa kuwataka wasitoe msamaha kwa kodi kwa kampuni ya Alex Sterwart hatua
ambayo iliisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Via>>ITV
SHARE