Home Audio MAJANGA YA BVR KAHAMA !! 7 MIKONONI MWA POLISI, WAMO WALIOANDIKISHA WATU...

MAJANGA YA BVR KAHAMA !! 7 MIKONONI MWA POLISI, WAMO WALIOANDIKISHA WATU CHUMBANI KWA MTU USIKU, WENGINE KWA KUFANYA MAANDAMANO

SHARE

Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wane akiwemo mwenyekiti
wa mtaa wa Nyakato na kamanda wa sungusungu ambaye ni wakala wa UKAWA
kwa tuhuma za kuandikisha wapiga kura kinyume na taratibu usiku saa nne
na nusu katika mtaa wa Nyakato wilayani Kahama mkoani Shinyanga. 
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga na
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha tukio hilo
limetokea Juni 30,2015 saa nne na nusu usiku katika mtaa wa Nyakato,kata
ya Nyasubi wilayani Kahama. 
Kamanda
Kamugisha amewataja watu wane waliokamatwa  ni Nicholaus Kashanga
Azalia Mbwambo( 40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato,Kamanda wa
jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA katika zoezi la kuandikisha
wapiga kura. 
Wengine
ni Amos Elias (25),mkazi wa Mhongolo( BVR Operator),Mayunga Alphonce(
54) ambaye ni mwenyekiti wa mtaa Nyakato na mkazi wa mtaa huo na Lugina
Misango( 40) ambaye ni mratibu elimu kata ya Nyasubi. 
Kamanda
Kamugisha amesema watu hao wanaohojiwa na jeshi la polisi kuhusiana na
tuhuma za kuandikisha wapiga kura kinyume cha sheria,ambapo watu hao
wanatuhumiwa kuandikisha wapiga kura katika chumba anachoishi Nicholaus
Kashanga Azalia Mbwambo kwa kutumia mashine moja ya BVR usiku. 
Akifafanua
zaidi kuhusu tukio hilo Kamanda Kamugisha amesema kaika mashine hiyo
kumekutwa kadi tano ambazo zilikuwa zimechapishwa. 
“Katika
maelezo ya awali watuhumiwa wanadai mashine mbili zilipelekwa katika
chumba hicho ambacho kiko katika nyumba ya Machanya Joshua kwa ajili ya
kuchajiwa….”,ameeleza Kamanda Kamugisha. 
“Pia
tumemkamata Innocent Byamungu( 77) Mrundi ambaye baada ya kuhojiwa
amedai kutoa Shilingi 5,000/= kwa Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo ili
aandikishwe lakini hakuandikishwa kwa madai aliamuriwa na Nicholaus
Kashanga Azalia Mbwambo aondoke kwa kuhofia kukamatwa”,ameongeza. 
Katika
tukio jingine watu wawili wamekamatwa na jeshi la polisi katika
halmashauri ya mji Kahama kwa kosa la kuandaa na kuongoza maandamano
yaliyohusisha vijana wapatao 80 wakipinga kuhamishwa kituo cha
kuandikisha wapiga kura. 
Kamanda
Kamungisha amesema tukio hilo limetokea Julai 03,2015 saa nne na nusu
asubuhi katika ofisi za mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa
Kahama,ambapo Mary Issaack Sumuni(49) na Thobias Simon (36) wakazi wa
Majengo walikamatwa kwa kuandaa na kuongoza maandamano hayo. 
“Watu
hawa waliandaa na kuongoza maandamano kutoka mtaa wa Majengo hadi ofisi
za mkurugenzi bila kibali,walikuwa wanapinga kuhamishwa kituo cha
kuandikisha wapiga kura kutoka Uwanja wa Halmashauri ya mji kupelekwa
eneo la Maduka Kumi kwa madai kuwa watu wengi walikuwa bado
hawajaandikishwa”,amefafanua kamanda Kamugisha. 
Aidha amesema maandamano hayo yalisababisha kazi katika ofisi za mkurugenzi huyo kusimama kwa muda. 
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga anawaasa wananchi kufuata utaratibu
uliowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi katika kujiandikisha.
SHARE