Home Audio
SHARE

Kingunge
Ngombare Mwiru, ambaye ni kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
ametabiri anguko na mpasuko mkubwa ndani   chama hicho katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu, endapo chama hicho  kitaacha kumpitisha mgombea urais
anayekubalika kwa wananchi wengi.

Kauli
hiyo imekuja mara baada ya jina la Edward Lowasa kuenguliwa kutoka
majina matano  yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa (CC- NEC).
Kutajwa
kwa majina ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Amina Salum Ali,
January Makamba na Dk. Asha-Rose Migiro na Kamati kuu kwamba ndio
watajadiliwa na Halmashauri Kuu (NEC), kumemfedhehesha Kingunge hata
kusema, “…hatua ya kwanza itakuwa kumweka mgombea ambaye hakubaliki
ndani ya chama na hakubaliki nje ya chama. Itakuwa ni kura ya hasira.”
Kingunge ametoa kauli hiyo kwa kusitasita huku akionekana kuwa na huzuni wakati akifanya mahojiano na kituo cha Azam Tv  leo mchana.
 
Japo
Kingunge hakutaja jina la Lowassa lakini ni muungwa mkono katika mbio
zake za kuusaka urais  hata wakati wa mkutano wa kutangaza nia mjini
Arusha Kingunge alisema, “…Lowassa ndiye pekee anasifa za kuwa rais wa Tanzania.”
 
“Utaratibu
wa mwaka huu una matatizo. Kilichotokea ni mazingira yanayotia shaka.
Kwa sababu ya muda hakuna atakae kata rufaa. Inaonesha kwamba uongozi
umeshakuwa na msimamo juu ya mgombea wanaemtaka,”
amesema Kingunge.
 
Amesema kazi ya CC-NEC ni kuyapitia, kuangalia sifa, kuwapima, kuyalinganisha na kisha kutoa mapendekezo. “Hawana madaraka ya kuamua.”
 
Kuhusu kukubalika kwa majina hayo na NEC, Kingunge amesema, “…wajumbe
wa NEC wanaweza kukubaliana nayo, wanaweza kusema hapana, wanaweza
kusema wote waliopendekezwa hawafai na wanaweza kutoa mapendekezo
waletewe majina mengine.”
 
Amesema
kuwa yanayotokea sasa na yatakayotokea baadae ni mazingira ambayo
yamekuwa yakijengwa kwa muda mrefu na viongozi wakuu  wa  chama.
 
Kuhusu
sifa za mgombea anayemtaka, Kingunge amesema ni lazima: Aweze kupambana
na nguvu ya upinzani; anayekijua chama; awe na uzoefu wa masuala ya
ulinzi na usalama na mtu atakae watoa watanzani  kwenye umasikini.
SHARE