Home Audio
SHARE

 Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.
Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya
Segerea,  Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea
kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake Segerea
jijini Dar es Salaam jana na watu wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia
ni jamaa yake Martin Pemba.
Na Dotto Mwaibale
WATU wasiojulikana wamejeruhi kwa
mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea Steve Massaburi usiku
wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake alipokua akirejea kutoka matembezini.
Kwa mujibu wa Steve aliyelazwa katika
Hospitali ya Aga khan, watu hao wapatao wanne wakiwa na Pikipiki,
walimvamia majira ya saa tatu usiku nje ya geti la nyumba anayoishi na
kuanza kumshambulia huku yeye akijaribu kupambana nao.
Steve ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la
Dar es salaam Dk. Didas Massaburi, alisema wakati watu hao
wakimshambulia walikuwa wakisema wazi wazi kuwa lengo lao ni kumuona
hagombei nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya Segerea baada ya yeye
kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo.
“Walikuwa wakiniambia kuwa wewe si
unautaka udiwani sasa utaugombea ukiwa kitandani au kaburini, hapa
hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa kila mtu anaitaka nafasi hiyo”
alisema Massaburi.
Alisema wakati akiendelea kupambana na
watu hao alikuwa akipiga kelele jambo lililowafanya watu hao kumuacha na
kasha kukimbia huku yeye akiwa amelala chini damu zikimtoka sehemu za
shavuni kutokana na panga alilopigwa.
Pamoja na sehemu ya shavuni, watu hao
pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali za mkono wake wa kushoto alipokuwa
akijaribu kuzuia panga kumdhuru sehemu za usoni.
“Kelele nilizopiga ndizo zilizonisaidia
kwa kuwa ziliwafanya watu watoke katika majumba yao kuja kunisaidia
wakati huo huo watu hao wakikimbia kwa kutumia pikipiki zao mbili
walizokuwa wamekuja nao” aliongeza.
Alisema kwa sasa hali yake inaendelea
vizuri  tangu alipofikishwa hospitalini hapo jana huku akishonwa nyuzi
zaidi ya ishirini katika taya lilipigwa na panga na watu hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
SHARE