Home Audio JONAS MKUDE AREJEA BONGO KIMYAKIMYA TOKA AFRIKA KUSINI….

JONAS MKUDE AREJEA BONGO KIMYAKIMYA TOKA AFRIKA KUSINI….

SHARE
Mkude pic
Jonas Mkude tayari amerejea
nchini Tanzania akitokea Afrika Kusini ambako alikwenda kufanya
majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits FC inayoshiriki ligi kuu (PSL) ya
nchini humo.
Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba, kiungo huyo wa Simba ameshindwa kufaulu kwenye majaribio hayo.
Afisa habari wa klabu ya Simba
Hajji Manara amesema bado hajapata taarifa yoyote ya kufaulu au kufeli
kwa Mkude kwenye majaribio aliyokuwa akifanya kwenye klabu ya Bidvest
Wits ya Afrika Kusini. 
“Sijapata hiyo taarifa kiukweli,
Jonas yupo na timu lakini sijapata taarifa kwamba mefeli au amefaulu
kwasababu nikikuwa na pilika nyingi za ‘Ramadhani’ na sijasoma vyombo
vya habari kwahiyo siwezi kusema lolote”, amesema Manara.
Timu (Simba) imeondoka juzi
kuelekea Lushoto kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao kwahiyo siwezi
kujua ‘position’ yake mpaka leo nitakapokuwa ofisini ndipo ntaweza
kulitolea tamko”, ameeleza.

source:
shaffihdauda.co.tz

SHARE